Taifa Tanzania
Taifa Tanzania. Gazeti Huru la Afrika Mashariki linaloandaliwa kwa lugha ya kiswahili

Faru wa Mwana wa Mfalme wa Uingereza Apata Mjukuu katika Hifadhi ya Mkomazi

Faru Jike ajulikanaye kama Grumeti, ambaye awali alikuwa akiishi nchini Uingereza kabla ya kuhamishiwa Tanzania, amepata mjukuu.

Grumeti, kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Emmanuel Moirana ni moja ya Faru wawili walioletwa nchini mwaka 2012, na ambao Mwana wa Mfalme wa Uingereza, Prince William amekuwa akiwafuatilia kwa karibu.

Faru mwingine aliyeletwa nchini ni Faru Zawadi ambaye pia kwa sasa nay eye ni Mama wa Watoto wawili. Ila Grumeti ndiye kapata Mjukuu.

Mwana wa Mfalme, yaani Prince William awali alikuwa akiwafuatiliwa walipokuwa nchini Uingereza katika hifadhi maalum ya Port Lympne Safari Park iliyoko eneo la Kent.

Mara baada ya kufika Mkomazi, Mkoani Kilimanjaro Faru Grumeti, alipata mtoto wa kike aitwaye Mobo aliyezaliwa mwaka 2016.

Ilipofika mwezi Septemba mwaka 2028, Mwana wa Mfalme, Prince William alifunga safari kuja nchini Tanzania kumuangalia Faru huyo mpya aitwaye Mobo.

Prince William alipokuwa nchini alipiga kambi kwenye hifadhi ya Mkomazi kwa Zaidi ya Siku Tatu akiwafuatilia wanyama aina ya Faru wanaotunzwa katika mradi maalum hifadhini humo.

Hivi sasa, ni huyo Faru Jike aitwaye Mobo, ambaye na yeye amepata mtoto.

Faru huyo mpya nchini kiuhalisia ni Mjukuu wa Grumeti Faru ambaye Mwana wa Mfalme wa Uingereza huwa anamfuatilia sana huku Tanzania.

Mwingine, lakini mtoto huyo aliyepatikana Mwanzoni mwa Mwezi Machi bado hajapewa jina.

“Kwa kawaida watu huwa wanalipia ili Faru wapewe majina yao,” alisema Mhifadhi Moirana.

Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa Hifadhi ya Mkomazi kumpa Faru huiyo mtoto jina la mmoja wa wanafamilia ya Mfalme Charles III wa Uingereza kwa sababu Mwana wa Mfalme, Prince William ni mdau mkubwa wa Mradi wa Faru, Mkomazi.

Kutokana na hali hiyo, wafuatiliaji wa masuala ya uhifadhi wanatabiri kuwa kuna uwezekano wa Faru huyo mtoto kuitwa Kate, Princess of Wales ambalo ni jina na mke wa Prince William.