Taifa Tanzania
Taifa Tanzania. Gazeti Huru la Afrika Mashariki linaloandaliwa kwa lugha ya kiswahili

Jamnalal Bajaj: Uvumbuzi wake unavyoibadilisha sekta ya usafiri Tanzania

Hivi karibuni, mfumo wa usafiri katika miji ya Tanzania ulianza kuchukua mfumo mpya.

Pikipiki zenye magurudumu matatu zimeingia ghafla na kwa wingi katika biashara ya kusafirisha abiria mijini.

Pikipiki hizo ni pamoja na Bajaj kutoka India na TVS kutoka China.

Ni vyombo vya usafirishaji katika miji ya Tanga, Mbeya, Moshi, Arusha, Morogoro na hivi sasa, jijini Dar-es-salaam pia.

Chimbuko la pikipiki hizi za “miguu mitatu” hasa ni kule nchini India katika kampuni ya Bajaj.

Ni kampuni iliyoanzishwa na Jamnalal Bajaji ambaye ubunifu wake sasa unaelekea kubadilisha muelekeo wa usafiri Tanzania.

Jamnalal Bajaji alizaliwa nchini India mwaka 1889. Alifariki mwaka 1942.

Akiwa na umri wa miala mitano tu aliasiliwa katika familia moja tajiri nchini India.

Familia yake hiyo ya kufikia hasa ndio iliyokuwa ikijishughulisha na biashara na akapitia njia hizo.

Inaelekea aliishi vizuri katika familia hiyo na pengine ndio maana akazoeshwa shughuli za biashara.

Akawa mfanyakazi kwenye maduka ya familia. Na pia kushirikishwa katika kilimo Cha pamba.

Kijana Jamnalal aliweka akiba na mwaka 1926 alifungua kampuni yake iitwayo Bajaj Group ambayo ndani yake kuna kampuni ya Bajaj Auto.

Hii BAJAJ AUTO ndimo ilipobuniwa pikipiki ya matairi matatu (tri-motorcycle).

Pikipiki hiyo ya matairi matatu kwetu huku imezoeleka kwa jina la BAJAJ ingawa kuna pia TVS kutoka China na nyingine kadhaa.

Kampuni hiyo inaunda pia pikipiki za kawaida na zile zinazojulikana kama ‘Scooter.’

Pikipiki maarufu aina ya ‘Boxer,’ pia hutengenezwa na kampuni ya Bajaj.

Vile vile kampuni hiyo hutengeneza injini za boti ndogo.

Jamnalal anatajwa kuwa mmoja kati ya wawekezaji wakbwa katika viwanda nchini humo.

Katika orodha yumo Jamshendji Tata mwanzilishi wa kampuni ya TATA GROUP iliyobuni magari ya abiria yenye milago miwili ubavuni.

Pamoja na uwepo wa TVS za China ambazo kwa Tanzania ziko kwa wingi zaidi, Bajaj Auto inabaki kuwa ndio kampuni namba moja duniani kwa uzalishaji wa pikipiki za matairi matatu.