Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Kwa nini Kisiwa kinachoelea katika Ziwa Nyasa huitwa Falkland?

Hapo zamani palikuwa na Wanyasa wenye kufuatilia mambo mbalimbali duniani kote, hasa kupitia mawasiliano ya redio.

Wazee wa sasa wanapenda sana redio kuliko televisheni.

Redio ziliwasaidia kujua mengi na kukuza ufahamu na kutunza kumbukumbu nyingi zaidi vichwani mwao. Moja ya kumbukumbu hizo ni Kisiwa kidogo cha Falkland kilichopo katika mpaka wa Njombe na Ruvuma katika Wilaya za Nyasa na Ludewa.

Ni juu ya ziwa Nyasa. Ziwa lililopo katika ya nchi za Tanzania na Malawi.

Sasa ni kwa nini paliitwa Falkland?

Rudi nyuma miaka mingi iliyopita. Yapata mwaka 1690 Kepteni John Strong wa Uingereza aliendesha meli ya Serikali kutoka Uingereza hadi kusini mwa bara la Amerika ya Kusini.

Kusini mwa Agentina katika bahari ya Atlantic.

Kepteni John Strong alitia nanga katika eneo lenye visiwa vikubwa viwili na visiwa vingine vingi vidogo kuzunguka eneo hilo.

Sijui wenyeji walipaita vipi kabla ya ujio wa meli ya Uingereza ikiongozwa na Kept. John Strong.

Yeye alipowasili hapo alifanya mpango pawe koloni la Uingereza. Akapaita Falkland.

Kuna East Falkland na West Falkland na visiwa vingine vingi vidogo zaidi ya 700 kuzunguka eneo hilo. Vyote kwa ujumla huitwa Falkland.

Kepteni John Strong tayari aliweka mikakati ya eneo hilo kuwa sehemu ya Uingereza.

Umbali kutoka Uingereza hadi Falkland ni mrefu na kwa meli ni safari ya siku nyingi, wakati safari kutoka Agentina hadi hapo Falkland ni fupi.

Basi Aprili 1982 palizuka vita baridi kati ya Uingereza na Agentina. Kila mmoja alidai kuwa Falkland ni mali yake. Lakini mwishoni Falkland ikaendelea kuwa mali ya Uingereza.

Na wakati huo katika mpaka wa Njombe (zamani Iringa) na Ruvuma katika Wilaya za Nyasa (zamani Mbinga) na Ludewa pana kisiwa kidogo na kila upande ukidai kuwa ni mali yake na hivyo kusababisha ugomvi katika uvuvi.

Hapo panajulikana kuwa na samaki wengi wakubwa na watamu duniani kote. Naam, ni watamu sana.

Ili kuepuka ugomvi mkubwa zaidi ambao pengine ungeleta matatizo makupande zote mbili, wazee wale wakati huo ilibidi watumie Diplomasia yao ili kulifanya eneo la kisiwa hicho liwanufaishe watu wa pande zote mbili bila mgogoro wowote.

Basi kwa Diplomasia waliyotumia waliamua kukipatia jina jipya kisiwa hicho. Kikaitwa Falkland wakirejea mgogoro wa Uingereza na Agentina kugombea kisiwa cha Falkland, Kusini mwa Agentina katika bahari ya Atlantic.

Hadi sasa kisiwa hicho kidogo katika ziwa Nyasa kinaitwa Falkland. Ni eneo lililoinua maisha ya wengi kupitia uvuvi.

Falkland ya bahari ya Atlantic Kusini mwa Agentina ina uongozi wake lakini kiongozi mkuu mfalme wa Uingereza. Hapo Falkland unaambiwa kwamba kiwango cha watu kutokuwa na ajira ni asilimia moja tu kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni. Ni kisiwa tajiri.

Utajiri wa Falkland ulitokana na uvugaji wa kondoo kibiashara. Hasa manyoya yake yalikuwa yakiuzwa sana na kuongeza pato la nchi.

Lakini ujio wa viwanda vya kutengeneza nyuzi za nguo (synthetic fibres) uliangusha biashara ya sufu (manyoya ya kondoo) na hivyo Serikali ikabidi itazame chanzo kingine cha mapato.

Basi uvuvi wa kisasa ikapewa nafasi na hivyo yeyote aliyehitaji kuvua kibiashara alipewa kibali na Serikali ya Falkland.

Sasa Agentina ikaona hapana, majirani watakulajd samaki waliopo jirani kabisa na kwetu, wanazalisha na samaki wetu. Basi kila mmoja akadai kuwa Falkland ni mali yake. Na huko ziwa Nyasa palitokea jambo la aina hiyo na kuitwa Falkland.

Habari Zingine
Tuachie majibu

Anwani yako ya Email haitaonekana