Habari, Utamaduni, Historia na Simulizi za Tanzania na Afrika Mashariki

Marekani kuendelea kushirikiana na Tanzania katika katika Juhudi za kuhifadhi Maliasili nchini

23

Marekani imesisitiza kuwa itaendelea kudumisha ushirikiano na taifa la Tanzania katika kufuatilia, kulinda na kuhifadhi maliasili nchini.

Kiongozi wa Idara ya mazingira na usimamizi wa Maliasili kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID), Nathan Sage amesema kuwa sekta ya maliasili pamoja na kusaidia kuweka mazingira katika hali ya ubora, pia ni eneo muhimu katika kukuza uchumi na pato la taifa.

Sage alikuwa akizungumza jijini Arusha wakati anakabidhi vifaa maalum vya ufuatiliaji na utafiti wa wanyamapori kwa ajili ya taasisi ya kitaifa ya utafiti yenye makao yake makuu katika kanda ya kaskazini.

Taasisi hiyo ya Utafiti wa  Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) imepokea vifaa vyenye thamani yaTsh. 242,000,000 kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani USAID kupitia  mradi wake wa Tuhifadhi  Maliasili.

Akizungumza katika hafla ya  makabidhiano iliyofanyikia Makao ya TAWIRI, Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ya TAWIRI Dkt. David Manyanza ameishukuru USAID kutoa vifaa ambavyo ni muhimu  katika tafiti za wanyamapori  hususan sensa ya wanyamapori ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili hadi mitatu.

“Kama alivyowahi kusema Hayati Rais Ali Hassan Mwinyi, mali bila daktari  hupotea bila habari hivyo  hatuna budi kufanya sensa maalum za mara kwa mara ili kujua idadi wanyamapori nchini,” alisema Dakta Manyanza.

Mwenyekiti huyo wa bodi alibainisha kuwa hiyo ni njia mojawapo ya kuwa na uhifadhi endelevu wa wanyamapori nchini.

Manyanza amesema vifaa hivyo vina mchango mkubwa kwenye sekta ya Maliasili kwani tafiti za TAWIRI zinasaidia kuzishauri  mamlaka za uhifadhi.

“Ninatoa wito kwa tasasisi, mashirika na wadau wengine zaidi kujitokeza kushirikiana na TAWIRI ili kuwezesha tafiti za wanyamapori kwa ustawi wa  uhifadhi na  kukuza utalii ” ameeleza Dkt. Manyanza.

Kiongozi wa Idara ya mazingira na usimamizi wa Maliasili kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID), Nathan Sage, amesema kwa miaka 60 sasa, USAID imekuwa ikishirikiana Tanzania kuhifadhi bioanuwai  ikizingatiwa Tanzania ina utajiri mkubwa wa rasilimali  za kibaolojia ikiwemo maliasili ya Wanyamapori  ambao wana thamani kubwa ya kitamaduni, kiuchumi na  kielimu.

Sage ameongeza kuwa  katika kuendeleza ushirikiano huo, USAID  imetoa vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 242 kwa TAWIRI ili kuimarisha uhifadhi kwa kuwezesha matumizi ya teknolojia kurahisisha tafiti za wanyamapori

Kwa upande  wake  Mkurugenzi Mkuu TAWIRI  Dakta Eblate Mjingo amesema Jukumu kuu la TAWIRI ni kufanya tafiti za wanyamapori ambapo ameishukuru USAID kutoa vifaa ambavyo ni Kamera za kufunga kwenye ndege wakati wa kuidadi wanyamapori, Mikanda ya visukuma mawimbi ya Tembo (GPS Collars) na Vifaa vya Majira  nukta (Location GPS)

 “Utafiti ni gharama, unahitaji  vifaa  na teknolojia, hivyo vifaa hivi tulivyopokea vinakwenda kusaidia sana hususani kwenye sensa ya wanyamapori.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari