Taifa Tanzania
Taifa Tanzania. Gazeti Huru la Afrika Mashariki linaloandaliwa kwa lugha ya kiswahili

Nyambizi: ‘Meli’ ya Kutisha Bahari Kina ambayo sio hasa Meli bali ‘Ndege Maji!’

Nyambizi ni kama popo. Sio meli wala ndege

Mtambo ya aina hii inaitwa nyambizi na kwa kiingereza ni submarine.

Hizi nyambizi hasa ni kama ndege za chini ya maji ingawa watu huwa wanadhani kuwa ni aina ya meli.

Ingawa nyambizi ni vyombo vya majini na hupita hasa kwenye kina kirefu na vilindi vya bahari, hizi Submarine sio meli.

Labda jina sahihi linaweza kuwa “Ndege maji,’ au ‘Ndege Bahari,’ maana muundo wake ni kama ndege ila tu, yenye hupita chini ya maji.

Hiki chombo kinatumika Sana sana katika operesheni maalum, hususan za kijeshi au uokozi na pia katika kufanya upelelezi wa siri.

Nyambizi hupatikana kwenye bahari kuu (ocean) bahari ya Kadri (deep seas) na pia kwenye maziwa makubwa (great lakes) hasa yale ya ughaibuni.

Na Kwa sababu ni chombo cha bahari kina, Nyambizi hupitia ndani ya kina cha chini sana cha maji na wakati ikiwa safarini huwa haionekani hadi inapoibukia juu.

Nyambizi huweza kupita chini ya meli bila kujulikana na hata maeneo ya pwani zenye vilindi virefu, mbali na katikatia za bahari kuu.

Hiki chombo nyambizi huwa kina kazi nyingi sana.

Kwanza kabisa Nyambizi hutumika na vikosi vya jeshi la wanamaji au ‘Navy,’ katika matukio ya kivita au doria, na wakati mwingine kwenye matukio ya upelelezi au spying.

Nyambizi pia hutumika kama silaha. Zinaweza kurusha mabomu, makombora au roketi kutoka kina cha bahari hadi angani au sehemu lengwa nchi kavu.

Za zingine huwa na misumeno maalum (torpedo) ya kutoboa au kukata meli na manowari za kivita na hatimaye kuzizamisha.

Mara nyingi hizi nyambizi huwa haziwezi kushambuliwa kirahisi zikiwa na bodi ngumu isiyoweza kul;ipuliwa kwa mabomu ya kawaida.

Ili ziweze kuharibiwa labda ziwe katika mashambulizi na nyambizi zingine.

Nyambizi zikiwa majini hutisha.

Na vyombo hivi huwa havitumii mafuta bali huendeshwa kwa nguvu za Nyuklia.

Lakini mbali na vita chombo hiki pia hutumika kwenye shughuli za uokoaji wa baharini (deep sea rescuing) na vile vile katika kufanya utafiti wa mambo ya baharini.

Sio kila nchi duniani inaweza kumiliki nyambizi. Hata Tanzania haina kifaa hicho.