Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Jinsi ya Kugundua Kamera za Siri zilizotegwa katika Nyumba za Kulala Wageni

Kadri teknolojia inavyokua, faragha inaendelea kuwa kitu adimu duniani kote.

Na maeneo ya nyumnba za kulala wageni kama Lojingi, Hoteli na Guest House zimnekuwa ni tatizo kubwa katika kuvujisha siri za wateja wake.

Ukiwa hotelini au nyumba ya kulala wageni utajuaje kama hakuna kamera ya siri yenye lensi ndogo ukubwa wa ncha ya pini?

Unaweza kusafiri kwenda mahali ambapo si mwenyeji kabisa, eidha kibiashara au kwa shughuli nyinginezo na kisha ukachukua hoteli au nyumba ya kulala wageni lakini pasipokujua, ukajikuta unachukuliwa picha mnato au video kwa usiri.

Katika kizazi hiki chenye vifaa maridadi vya kurekodia, vyenye kipimo kidogo cha ncha ya pini, unapaswa kuchukua tahadhari kwa kuzingatia mambo yafuatayo;

Ukiingia katika chumba cha hoteli au nyumba ya kulala wageni, zima taa za chumba kisha funga madirisha yote na utandaze mapazia. Washa kamera ya simu yako bila kuwasha mwanga wa kamera ya simu (flashlight).

Zunguka kwenye chumba huku ukikagua kuta na dari kwa kutumia simu yako ambayo imewashwa kamera bila mwanga (flashlight). Fanya zoezi hili bila kurekodi chochote.

Kama chumba kina kamera ya siri, utaona doti au alama ya mwanga au mwale mwekundu mdogo sana kwenye kioo cha simu yako.

Mahali ambapo doti au mwale huo unatokea ndipo lilipo jicho la kamera ndogo sana ya siri. 

Kama hakuna mwale wowote basi chumba kiko salama kabisa kukitumia.

Si tu kamera hufichwa kwenye kuta za chumba,  lakini pia hufichwa kwenye taa za chumba.

Siku hizi za teknolojia iliyoboreshwa zaidi, ukusanyaji wa taarifa hufanywa kwa kificho sana.

Unavyoingia tu ndani ya chumba cha nyumba ya kulala wageni/lodge/hotel zitazame taa zilizotumika kukupa mwanga wakati wa giza. 

Si kila taa unayoiona ndani ya chumba imewekwa kukupa mwanga, nyingine huwekwa kwa siri sana ili kurekodi matukio ndani ya chumba husika.

Taa hizi huwekewa camera ndogo sana ambayo itaanza kurekodi mara tu utakapowasha taa hizo zenye kamera. Zikague taa hizo kama ulivyofanya kwenye kuta.

Kama zina kamera basi utazijua kwa kuuona mwale wa mwanga. Kama zipo umbali mfupi kuzifikia, unaweza pia kuzitoa kwa umakini na kuzikagua iwapo una uzoefu na taa zenye kamera.

Zingatia haya

Camera ya simu yako kupitia screen yake, ina uwezo wa kuuona mwale wa kamera nyingine ambayo inarekodi kwa siri sana.

Kamera nyingi za siri hurekodi kwa kuzalisha mwale wa mwanga ambao macho yetu ya kawaida hayawezi kuona, ni kama vile ule mwale unaozalishwa kwenye jicho la remote controller ya TV, ni vigumu kuuona lakini jicho la kamera iliyowashwa likielekezwa mbele ya remote inayobofywa, bas ule mwale huonekana waziwazi.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari