Habari, Utamaduni, Historia na Simulizi za Tanzania na Afrika Mashariki

Wanawake Tanzania ni Wapenzi na vile vile Wahanga wa Mitandao ya Kidijitali kwa Wakati Mmoja

14

Huku ikielezwa kuwa wanawake ndio wanaoongoza katika matumizi na ufuatiliaji wa Mitandao ya kijamii kupitia simu janja, taarifa za upande wa pili zinaonesha kuwa kundi hilo pia ndio wahanga wakubwa wa matukio ya uhalifu wa kidijitali.

Ukuaji wa wa sayansi na teknolojia umechangia sana suala la utandawazi na ongezeko la simu janja pia matumizi tofauti tofauti ikiwemo mitandao ya kijamii.

Hatari na Athari za Mitandao

Moja ya kundi kubwa linalotajwa katika kasi ya utumiaji wa mitandao ya kijamii ni wanawake ukiachilia kundi jingine la vijana

Wanawake hasa wa kisasa wamekuwa watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii kiasi cha kufikia kuposti hadharani faragha zao, zikiwemo piacha au video za familia na hata maisha yao binafsi hasa katika malezi ya watoto

Imekuwa ni mtindo wa kisasa kwa wanawake kuweka taarifa za watoto wao katika mitandao ya kijamii kabla ya umri wao pasipo kufahamu kuwa wanawaharibu watoto kisaikolojia hasa wanapo kuwa wakubwa.

Baadhi ya wanawake wamekuwa wakitumia mitandao hiyo kuweka picha za watoto wao katika sherehe mbali mbali mfano sherehe za kuzaliwa, huweka picha mbali mbali za kumbukizi  zinazoendana na siku hiyo mfano mtoto amevaa pampas, mtoto akiwa mchanga na kadhalika.

Tamko la Mamlaka ya Mawasiliano

“Wanawake wanachangia Sana katika mmomonyoko wa maadili wanawake wengi wanalea watoto kwa kuiga maisha ya mtandaoni.”

“Mbaya zaidi watoto wananunuliwa simu kitendo ambacho sio vyema kwa kuzingatia umri wao na kupevuka kwa akili.”

“Ni hatari kuwaachia watoto wawe wanatumia simu janja na kuingia mitandaoni bila usimamizi. Kwani kwa kufanya hivyo mtoto anaweza kushuhudia matendo machafu pamoja na kujifunza  tabia zilizo kinyume na maadili. Pia si ajabu na yeye akaanza kuiga vitu anavyoviona kwenye picha na hata video! ”

Francis Mihayo – Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Kanda ya Kaskazini

Francis Mihayo alitoa angalizo hiyo hivi karibuni katika uzinduzi wa chama Cha wanawake waandishi wa habari Arusha (Arusha women in media) katika ukumbi wa Bunge la Afrika mashariki (EAC)

Sheria ya makosa ya mtandaoni Tanzania  ya mwaka 2015 (The Cybercrime Act 2015) inaeleza namna ya matumizi sahihi ya mitandao yakijamii ikiwemo kuweka picha na video za maadili kwa watanzania.

Pia Sheria ya mtoto Tanzania ya mwaka 2009 inaeleza namna mtoto anatakiwa alindwe,aheshimiwe na kupewa haki zake.

Ikumbukwe kuwa mitandao ya kijamii haisahau Mara mtoto atakapo kuwa mkubwa na kuona picha zake ziko mtandaoni zitamnyima Uhuru maana hatujui anaweza kuwa nani badae.

Suala hili la kubadilika kwa malezi  limeibua hisia tofauti kwa Bibi na mama zetu ambao kipindi Chao malezi yalikuwa tofauti na kuwashangaa wanawake wanao fanya hivyo.

” Mimi nashangaa Sana kuona wanawake wanaweka maumbile yao mtandaoni nasikia aibu Sana kumuona mwanamke ameweka picha yake ya ujauzito mtandaoni tena ameshikilia tumbo ili tuone, sisi enzi zetu tunakua  ujauzito ulikuwa unafichwa lakini Sasa hivi mtu anajipiga picha anaweka haoni hata aibu,” Mama Roserian Leizer, anaongeza.

Ikumbukwe kuwa mitandao hutunza kumbukumbu kwa kipindi kirefu na hata milele hivyo watoto au wajukuu wanaweza kuja kujionea vituko vya wazazi wao hapo baadae.

“Wanawake wamesahau wajibu wao wa kulea unakuta mwanamke ameshikilia simu muda wote hajui mtoto ameshinda wapi au kafanya nini hasa hawa watoto wa shule za sekondari na msingi ndio wako hatarini usipo wafuatilia utakuta wameshaharibika,” Gloria Massawe anabainisha.

Lengo la matumizi bora ya mitandao ni pamoja na kulinda utu wa mtu, kuzuia mmomonyoko wa maadili,kuwalinda wa toto na unyanyasaji wote.

Hata hivyo zipo njia tofauti tofauti katika kupunguza athari za mmomonyoko wa maadili haswa katika suala la malezi, ikiwemo Kupunguza kuweka taarifa binafsi mtandaoni, Mfano picha za watoto au Ujauzito kwa akina mama.

Pia ni muhimu kuweka private setting katika mtandao unayotumia ili watu wasiweze kupata taarifa zako., kufunga kifaa cha mawasiliano kutumia neno gumu la siri ili kutunza faragha.

Wanao tumia vifaa kama tablet kubwa au kompyuta ni vyema kuzilinda kwa kinga za virusi (antivirus) na udukuaji (anti-spyware).

Pia unashauriwa kutafakari ulazima, usahihi, usalama na uhakika wa jambo lolote kabla ya kuviweka mitandaoni.

Sheria ya mtoto  namba 21 ya mwaka  2009 Tanzania bara inaelekeza Wazazi na walezi wana wajibu mkubwa wa  kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa na kuchukua hatua pale ambapo watoto wanaonekana kunyimwa haki zao.

Pia Wazazi, walezi na jamii wana wajibu wa kuhakikisha kwamba wanawaongoza watoto katika kutekeleza wajibu wao kikamilifu.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari