Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Zaidi ya Mitandao 600 ya Habari yaanzishwa nchini Tanzania

Idadi ya mitandao ya habari, yaani ‘Online Media,’ imeongozeka kufikia 600 nchini, kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Taarifa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano inabainisha kuwa pamoja na kuanzishwa katika siku za hivi karibuni, idadi ya mitandao ya tarakimu ya habari digital media imeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Baadhi ya mitandao hiyo pia, ikiwemo ‘Taifa Tanzania,’ kwa sasa imeanza kupenyeza katika wigo wa kimataifa.

Mitandao husika ni pamoja na Magazeti ya kwenye mitandao, Blogu Binafsi, Runinga pamoja na Redio za mitandaoni nyingi zikiwa zimeegemea kwenye jukwaa la YouTube.

Wakati huo huo, idadi ya vituo vya redio pia imeongezeka kutoka stesheni moja tu, iliyokuwepo wakati nchi inapata Uhuru, Desemba Mwaka 1961, hadi Zaidi ya stesheni za Redio 210 zilizopo sasa.

Na kipindi ambacho Tanganyika inapata Uhuru wake, Zaidi ya miaka 60 iliyopita, hapakuwa na stesheni yeyote ya Televisheni nchini, lakini sasa idadi ya vituo hivyo vya Runinga imefikia 54.

Inaaminika kuwa stesheni ya kwanza ya Televisheni, Tanzania Bara ilianzishwa mwaka 1994.

Vile vile idadi ya watumiaji wa intaneti nchini imeongezeka kufikia Zaidi ya asilimia 50 ya watanzania wote, kwa mujubi wa taarifa kutoka TCRA.

Hii sasa inamaanisha kuwa zaidi ya watanzania Milioni 30 wamefikiwa na huduma za mtandao wa intaneti, wengi wao wakitumia Zaidi simu za kisasa katika kuogelea kwenye mtandao.

Hilo ni ongezeko la Zaidi ya watumiaji Milioni 7 ndani ya kipindi cha chini ya miaka mitano, kutoka idadi ya watumiaji 23 milioni iliyoorodheshwa mwaka 2018.

Hata hivyo, ikilinganishwa nan chi zingine barani humu, kama vile Kenya, Nigeria na Afrika Kusini, idadi ya watanzania wanaotumia mtandao wa intaneti bado iko chini.

Pia, tovuti za Tanzania, hususan za masuala ya habari, bado ni chache sana ukilinganisha nan chi zingine.

Mwaka huu mamlaka ya mawasiliano Tanzania imeongeza kikoa kingine cha mtandao wa intaneti (domain extension) cha dot.tz.

Kwa sasa Tanzania itakuwa na vikoa viwili, kile cha awali cha dot.co.tz kilichodumu muda mrefu na hiki kipya cha dot.tz kilichoanza rasmi mwaka 2022.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari