Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

George Gathogo: Msindikaji Maziwa anayelenga kuteka soko la Afrika Mashariki

Kutana na Tatu Milk  kampuni mpya ya kutengeneza kinywaji kitokanacho na maziwa mtindi yaliyoongezwa ladha maalum, yaani Yogurt.

Tatu Milk ilianzishwa hivi karibuni nchini Kenya.

Ni kampuni ambayo pamoja na ugeni wake kwenya sekta hii, ambayo imefanikiwa kuvuka viwango vya kawaida vya kibiashara kwa kuibuka mshindi wa jumla katika sekta ya usindikaji na utengenezaji bidhaa zinazotokana na Maziwa halisi.

Mashindano hayo yaliandaliwa na taasisi iitwayo Kenya Beverage Excellence Awards .

George Gathogo  ndiye hasa mwazilishi mwandamizi wa Kampuni ya Tatu Milk inayozalisha bidhaa ya Yougurt maarufu kama Bogani Youghrt.

Hapa anaelezea jinsi ambavyo biashara hii ilivyoanza.

Na alianza kutengeneza Yogurt katika jiko lake la nyumbani kwake.

Sasa kwa mujibu wa Gathogo, biashara yake awali ilitakiwa kusimamishwa na kuzuiwa kuendelea.

Shirika la uhakiki wa ubora wa bidhaa inchini Kenya yaani KEBS liliingilia kati, kudai uzalishaji wa Yogurt ulikuwa haukidhi viwango.

Hii ni kwa sababu ya sheria inayotaka kuwa kila mwazilishi wa biashara yoyote ya uzalishaji  lazima awe na eneo maalum pamoja na kiwanda rasmi kinachokidhi ubora na vigezo vya uzalishaji.

“Kusema kweli safari yangu ya uzalishaji bidhaa za maziwa haikuwa rahisi kwani nimekumbana na changamoto nyingi,” anasema Gathogo.

Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na wafanyabiashara na wamiliki wa maduka kuzuiwa kuuza bidhaa zake.

Kingine ni suala la washindani wake kibiashara kuwatishia watu waliotaka kusambaza au kuuza bidhaa zake kwamba wangesitisha kumpa bidhaa zingine za maziwa kutoka kwao iwapo angeendelea kuchanganya maziwa yake na yao.

Mkurugenzi huyo wa kiwanda Cha maziwa anasema kuwa aliwaeleza maafisa kutoka kwa shirika la uhakiki wa bidhaa kwamba yeye alikuwa ni mjasiriamali mdogo asiye na mtaji mkubwa.

Na kuwa hata yeye angelipenda kuwa na kiwanda ila tatizo ni ukosefu wa fedha za kutosha kuwekeza kwenye kiwanda.

Hatua hiyo walau ilimsaidia kupunguza mvutano baina yake na maafisa wa serikali kuhusu yeye kukidhi vigezo vya uzalishaji.

Kwa mujibu wa Gathogo ni kwamba baadae sana biashara yake ilipata umaarufu wakati rafiki yake alipomuunganisha na afisa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa yaani UN.

Rafiki yake huyo alikuwa ni Raia wa Marekani ambaye alianza kuagiza bidhaa za maziwa kutoka kwake.

Na kadri alivyoendelea kununua bidhaa hizo kwa wingi, ghafla na watu wengine nchini Kenya pia walianza kuvutiwa kujaribu.

Na wengi waliyapenda maziwa yake na taratibu akawa anapata wateja na soko lake kuanza kukua.

Mkurugenzi wa Tatu katika mwezi wa Novemba ameweza kutunukiwa  Tuzo la mmiliki wa bidhaa nchini Kenya inqyopendwa Zaidi na watoto kupitia kampuni ya Kenya Beverage excellence Awards inayomilikiwa na Bwana Calvin .

“Ni kama muujiza vile, kuona kampuni inachipuka ndani ya mwaka Moja na kujipatia umaarufu mkubwa mno Hadi kufikia hatua inapendwa kiasi hiki hii haijawai kutokea hasa hapa nchini Kenya ambapo ushindani ni mkubwa mno.” anaongeza bwana Calvin mkurugenzi wa Kenya Beverage.

Januari 2023 George atakuwa anatimiza mwaka Moja katika uzalishaji wa Youghrt nchini Kenya.

Na anatarajia kuwa bidhaa hii itakuwa imeenea ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

George sasa anatoa ushauri kwa wajasiria Mali wanaoanzisha biashara zao kuwa wajasiri na Mali zao na pia kutoa with ya inawezekana kufanya biashara la msingi ni wazo na hata pia lengo.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari