Taifa Tanzania
Taifa Tanzania. Gazeti Huru la Afrika Mashariki linaloandaliwa kwa lugha ya kiswahili

CHADEMA kuwarejeshea tena wakazi wa Karatu Mradi wao wa maji

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimezindua rasmi mikutano yake ya hadhara wilayani Karatu.

CHADEMA imefanya mkutano mkubwa wa siasa katika viwanja vya mazingira bora vilivyopo katikati ya mji wa karatu, tukio ambalo limehidhuriwa na maelfu ya wakazi wa eneo hilo pamoja na vitongoji vyake.

Baadhi ya watu walisafiri kutoka Mto-wa-Mbu, Monduli na Ngorongoro ili kuhudhuria tukio hilo.

Chama hicho kikuu cha upinzani nchini kimezindua pia mikakati yake mipya mbalinbali ya kujijenga na kujimaarisha katika nyanja za siasa baada ya miaka nane bila kufanya mkutano wowote wa hadhara.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja vya mazingira bora, mwenyekiti wa chama hicho Samwel Welwel amesema kuwa baada ya uzinduzi wa mkutano huo watakuwa na mikutano kwa Kila kata.

“Lengo ni  kwa kusikiliza kero za wananchi ambao walikuwa na kiu ya muda mrefu ya kuzungumzia matatizo yao lakini wakishindwa kufanya hivyo kwa sababu mikutano, ambayo ni haki yao kikatiba, ilikuwa imezuiliwa,” alisema Mwenyekiti huyo wa wilaya.

Mkutano wa CHADEMA mjini Karatu

Welwel alitaja baadhi ya mikakati yao mipya kwamba ni pamoja na kujipanga kwa uchaguzi ujao wa serikali za mitaa 2024 na baadaye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa Chama Chake kitaikomboa wilaya ya Karatu na kuirudisha CHADEMA kwani hata hivyo ushindi wao wa mwaka 2020 uliporwa.

Alitaja mkakati mwingine kuwa Ni kuhakikisha bodi ya maji  ya mradi wa KAVIWASU uliovunjwa hivi karibuni nakuunganishwa kuwa bodi moja KARUWASA na  Waziri wa maji Juma Awesso unarudishwa.

“Mradi wa Kaviwasu ni mradi wa wananchi wa vijiji sita ambao walihangaika kuchimba mitaro kwa juhudi kubwa ili waweze kujipatia huduma hiyo,” alisema.

“Wananchi mnakumbuka  jinsi ambavyo mwaka 2000 kulikuwa na shida kubwa ya maji katika wilaya yetu ya Karatu?,” aliwauliza wakazi wa eneo hilo katika mkutano.

“Watoto wetu walikuwa wakiacha shule kwa kukesha  kwenye foleni ya kutafuta maji lakini Jimbo katoliki la Mbulu kwa kushirikiana na aliyekuwa mbunge wa Jimbo wakati ule Dokta Wilbroad Slaa waliwasaidia wananchi wa Karatu kwa kuleta mradi huo ambao ulikuwa msaada kwa wanawakaratu kwa kuondoa adha ya maji” alisema Welwel.

Aliongeza kuwa Jambo Hilo la kuvunjwa bodi na kuunganishwa kuwa bodi moja imekuwa na changamoto kubwa ikiwemo maji kuwa ya shida katika wilaya hiyo kwani Bei ya maji imepanda na  kurudi Kama miaka ya 2000 ya ndoo ya Lita 20 kuuzwa sh 500.

“Ndugu waziri wa maji tunakuomba urudishe bodi ya Maji ya KAVIWASU Kama zamani usiturudishe Kama zamani tulisahau shida ya maji Karatu Sasa umeturudisha tulikotoka” alisema WelWel.

Mmoja wa wakazi wa Karatu, Amsi John alilaani kitendo Cha bodi hizo kuunganishwa kwani Sasa maji yamekuwa ya shida kwao.

“Kwa sasa kuna foleni kubwa na wauzaji wanauza maji ya Lita 20 kwa shilingi Mia Tano Jambo ambalo limekuwa kero kwa watumiaji.”

“Hembu angalia Sasa foleni iliyoko kwenye bipi za maji tumerudi Kama zamani tunauziwa maji sh 500 ndoo haijawahi kutokea tangu KAVIWASU ilipoanza” alisema Amsi