Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Moitiko akabidhi Ng’ombe 50 na Mashine ya Kusaga Nafaka kwa miradi ya Wanawake Monduli

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi wilayani Monduli, Kisioki Moitiko ametoa Ng’ombe 50 na mashine ya kusaga kwa ajili ya kuwaunga mkono akina mama wa maeneo hayo katika nyakati hizi ngumu za ukame uliokithiri.

Aliwataka wakina Mama kuendelea kuunda vikundi maalumu kwajili ya kujiendeleza.

Huku akikiri kwamba ukame ni tatizo sio tu Monduli bali nchi nzima aliongeza kuwa ameamua kuwaunga mkono kwa kitoa takriban Ngo’mbe dume 50 na mshine moja ya kusaga.

Aliwataka waanzishe mradi wa unenepeshaji wa Ngo’mbe kutokana na mifugo hiyo.

Kuhusu Mashine hiyo ya kusaga alitake itumike Kuingiza kipato kwa Vikundi hivyo vya kina Mama pamoja na chama cha mapinduzi ngazi ya kata.

Wakati huo huo wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Esialalei wilaya ya Monduli wametakiwa kubuni miradi ya kimaendeleo itakayo wasaidia kujikwamua kiuchumi hasa katika kipindi hiki cha ukame mkali katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti huyo wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya Kisioki Moitiko alipotembelea kata hiyo akiwa katika mwendelezo wa ziara yake ya kata kwa kata yenye lengo la kufufua chama na kuwashukuru wanachama kwa kumchagua kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo.

Kisioki alisema Sasa ni wakati wa kuwa na siasa uchumi, ambapo ameitaka jumuiya hiyo na chama kwa ujumla wilayani humo kubuni miradi mbalimbali itayo waingizia fedha za kujiendeleza kiuchumi ili kuhimili khali ya mdororo wa uchumi na ukame ulio kumba maeneo mengi kote ulimwenguni.

“Nimekuja nyumbani wamenipokea vizuri na Marafiki zangu wamenipa zawadi za kutosha, kama mliivyoona nimepewa mbuzi zaidi ya arobaini na dume kadhaa, lakini nimeona na mimi niwape marafiki zangu ili wakina Mama nao wapate kwahiyo kila aliepata mbuzi naye atatoa dume kwajili ya kina Mama, kwaiyo natoa madume amsini kwa kina Mama ili kuendelea na mradi wa Unenepeshaji ” alisema Kisioki.

Awali akiwa njiani kuelekea Esilalei Mwenyekiti huyo amepitika katika kijiji cha Loseirwa kukagua Ujenzi wa Shule ya msingi unaoendelea na kukuta changamoto mbalimbali katika Mradi huo ikiwemo maji ya ujenzi na nishati ya kwajili ya Mwanga.

Hata hivyo, baada ya kusikia changamoto hizo aliahidi kutoa paneli za umeme wa nguvu ya jua (Sola) zenye Watts 60 Kwajili ya kuzalisha umeme jua.

Vile vile ameahidi kupeleka matanki makubwa sita ya maji pamoja yatakayotumika katika ujenzi wa madarasa hayo ya shule hiyo ya msingi ambayo ni ya pili sasa katika kata hiyo ya Esilalei baada ya Shule Mama “Shule nyekundu”

“Nimesikia risala na nimesikia changamoto zenu ikiwemo maji na umeme, kwa muda huu kwanza naomba niwatatulie swala la Maji na Nishati nitatoa Solar watts 60 na Maji Bowser 6 na zitaletwa na trekta yangu hapa kwanzia sasa hivi” alisema Kisioki.

Katika Ziara hiyo pia Wamehudhuria Viongozi Wengine akiwemo katibu wa Jumuiya hiyo Bi Beatrece Mandia Pamoja na Katibu Malezi, Elimu na Mazingira Ndugu, Thomass Meiyan ambapo kwa upande wake Bi Mandia Aliwaasa Wanachama wa CCM kuendelea Kujiandikisha na kuwa wanachama hai na wanaotambulika ili kufanikisha Uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2024/2025.

“Nimeona idadi ya Wanachama kwa kila tawi lakini idadi ya wanachama wa ccm ni kubwa zaidi kuliko idadi ya wanajumuiya, sasa nitoe rai kila mwana ccm lazima awe na kadi ya uanachama ili tumtanbue pia wale wote wenye sifa za kuwa wanajumuiya nawahasa sana mjiandikishe na mpate kadi zenu” alisema.

Nae Katibu Malezi, Elimu na Mazingira Ndugu Meiyan ametumia jukwaa hilo kuwataka wanachama na Wanachi wote kuwekea msisitizo na umakini katika malezi ya Watoto kwani Watoto wengi wapo kwenye hatari ya kuharibika kutokana na kuzidi kuongezeka kwa utandawazi

Aliwataka pia wazazi wote kwa pamoja kushirikiana katika malezi ya watoto kwanzia kwenda pamoja clinic mpaka mama atakapo jifungua kwani ushirikiano huo utasadia wazazi kumlea mtoti katika mazingira Salama zaidi na kuwa na taifa imara na makini.

Nao Viongozi na wanachi wa kata ya Esilalei Wilaya ya Monduli wameishukuru Mwenyekiti wa jumuiya hiyo kwa misaada hiyo aliyo wapatia wananchi huku wakimrai kuwa aendelee kufanya hivyo katika jamii ya wanamonduli wote.

Ziara ya Jumuiya hiyo ya wazazi ilianza mwezi February mwaka 2023 na inatarajiwa kuendelea mpaka mwezi Mach na ikiwa na malengo makuu mawili Mosi ikiwa kufufua chama na Jumuiya hiyo pamoja na kushukuru kwa uchaguzi.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari