Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

China na Tanzania zatimiza Miaka 58 ya Ushirikiano

Rais wa China alipozuru Tanzania miaka kumi iliyopita

China na Tanzania zinatimiza miaka 58 ya ushirikiano wa Kidiplomasia na viongozi wa nchi hizi mbili wanakutana jijini Beijing.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameanza ziara ya siku tatu nchini China.

Katika safari yake Beijing, Rais Samia, pamoja na masuala mengine ndio atakuwa na mazungumzo rasmi na kiongozi wa nchi hiyo Xi Jinping.

Ziara yake ya kikazi iliyoanza siku ya Jumanne ya tarehe 2 hadi 4 Novemba kufuatia mwaliko kutoka kwa Kiongozi wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping ambaye mwaka 2013 pia alitembelea Tanzania.

Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na kiongozi wa juu kutoka bara la Afrika tangu Rais Xi Jinping achaguliwe tena na Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China kuwa Katibu Mkuu kwa muhula wa tatu.

Vilevile, ziara hiyo itakuwa miongoni mwa ziara za mwanzo za viongozi wa kitaifa kutembelea nchini China tangu utokee mlipuko wa UVIKO-19 mwezi Desemba 2019.

Rais Samia anapokelewa rasmi katika ukumbi wa Great Hall of the People jijini Beijing.

Baada ya mapokezi Samia Suluhu Hassan atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa China, Xi Jinping.

Mbali na hayo, Rais Samia Suluhu atashuhudia utiaji saini wa mikataba mbalimbali kati ya China na Tanzania.

Pamoja na kukutana na Xi Xinping, Rais Samia pia anakutana na Waziri Mkuu wa China Li Keqiang.

Baada ya hapo Rais wa Tanzania atakuwa na mazungumzo na Spika wa Bunge la nchi hiyo Li Zhanshu.

Ziara ya Rais Samia inafanyika katika kipindi ambacho Tanzania na China zimeadhimisha miaka 58 ya mahusiano ya kidiplomasia.

Viongozi hao wawili wanatarajia kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano katika nyanja za siasa, uchumi, utamaduni na ushirikiano wa kimataifa.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari