Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Mahojiano Maalum na Mwanamuziki JB Mpiana

JB MPIANA ninani? Mpiana ni Mwanamuziki, mtunzi wa nyimbo na mwimbaji.

Kwa jina halisi anaitwa JEAN BEDEL MPIANA TSHITUKA, Lakini kwa nini aliitwa hivyo?

01) Nilipewa jina hilo la TSHITUKA kwamaana nimezaliwa nikiwa mtoto njiti.

Mimi ni Mtoto wa Mzee JEAN MPIANA WA MPIANA ambae kwa leo hii ni marehemu na Mama AGNES LUSAMBO FLORENCE TSHAME MUKINAYI.

02) Sitaki kuongelea swala la Watoto wangu kwenye TV, kwa maana Watoto wangu wote wanafahamika na hua nawaimba kwenye nyimbo zangu mara kwa mara.

Fahamu kwamba ninao Watoto wengi.

Mengine ni maisha yangu kibinafsi sipo radhi kuyaweka wazi kupitia media.

03) Kama ukiniona navaa nguo ya kifahari ilio bei ghali jua kwamba nipo kwenye shughuli yangu ya kazi.

Kwa hali ya kawaida utaniona navaa Jean’s.

04) Hadi kwa mda huu bado sijawa Babu, natamani saana kupata Mjukuu, Kijana wangu wa kwanza kama ananifwaya kwa mda huu basi ombi langu alifanyie kazi.

05) Muziki nimeuanza na Group WENGE, yaani sijawahi kupitia kwenye Orechestra yeyote.

Tulikua tukienda shule, baada ya shule tunakutana mtaani kwetu tunapiga muziki.

Mwanzoni Muziki kwetu haukua kama kazi hapana, ilikua kujifurahisha tuu.

06) Nilivyo fika shule sekondari kidato cha sita, sijafauli, na kwamaana kipindi kile ndo tumeanza kua Nyota wa Muziki, ndo nikawa nazembea kabisa kwenda shule.

Nachukua fursa hii kutoa shukran zangu kwa “WERRASON” maana nilikua sipendi tena kurudi shule, yeye ndo alikua akinihamasisha, yeye ndo kaenda kuniandikisha shule hadi nikafaulu kuhitimu kidato cha sita.

Mimi na ADOLPHE DOMINGUEZ tulihitimu mwaka mmoja shule moja.

Nikaingia chuo kikuu baada ya mwaka wapili chuo, ilinijia vigumu niendelee na chuo maana tumeshakua Ma Stars kupindukia..

Huwezi ukawinda sungura wawili kwa wakati mmoja, ikanibidi nichague Muziki ulivyo nifikisha hapa nilipo.

07) Swali lakujiunga kwangu na Group WENGE, sintoweza kubathilisha alicho kiongea Ndugu yangu WERRASON, yote kayaongea ndo ukweli mwenyewe.

Siku moja nikiwa nazunguuka kwenye mitaa ya Ndibaboma, nikawaona Jamaa wako wanaimba, niliungana nao bila kusita nami nikaanza kuimba, uimbaji wangu ukawashangaza wote.

Wakapigwa na butwaa kuona naimba kwa sauti ya kwanza.

Didier Masela alikuwepo, Alain Mwanga ZING ZING nae alikuwepo pia.

08) Nyadhifa ya Rais wa Group WENGE hapa nibora tuongee ukweli, kabla ya mimi kupewa Urais, alikuwepo Christian Nzitu.

Hapo bado hatujajitambua kabisa.

Kadri siku zinavyo songa ndipo tukaanza kujipanga nakujiwekea kanuni za Group.

Fahamuni kwamba wapo Watu ambao walijituma kwa hali na mali ili WENGE iwepo, na wapo wale ambao kutokana na WENGE wao wakajipatia umaarufu.

Kwa wale ambao walio jitolea ili wenge iwepo ndo sisi wakurugenzi 4 ndo tulikua tukiliendesha Group.

01) DIDIER MASELA (MKURUGENZI MUASISI WA GROUP)

02) ALAIN PRINCE MAKABA MKURUGENZI MASWALA YA KIUFUNDI

03) WERRASON MKURUGENZI MASWALA YA FEDHA

04) JB MPIANA MKURUGENZI RAIS WA GROUP

09) Ingawa nilikua Rais wa Group, sikua na mamlaka pekee na kamili kana kwamba naweza kuchukua maamuzi pekeyangu hapana, tulikua tukishirikiana wote kwa kila jambo.

10) Mtu wa kwanza kutusapoti kwa hapa ntasema mwanzoni tulikua tukijisapoti wenyewe kadhalika tulipata msaada kutoka kwa Ndugu zetu wa karibu.

Baadae akaja Mzee MAVO Mungu amlaze mahala pema, yeye katokea kutusapoti sana, yaani alikua nguzo imara kwetu.

Kwa hela zake katununulia hadi daladala tukiwa tunazunguuka nalo Jijini Kinshasa.

11) Show yetu ya kwanza ingawa hatujafaidika nayo kifedha nipale tulivyo tumbwiza kwenye Ukumbi wa OLYMPIA Jijini Kinshasa.

Baadae tukapata Mdhamini mwengine (TCHACHO MBALA KASHOGI) namtolea salaam zangu.

Yeye ndo katupeleka kufanya Show Mjini MBUJIMAYI, kwakweli tulipata pesa hadi tukachanganyikiwa.

Alicho kifanya kabla ya Show kuanza, kachukua Mike na katoa wito kwa Watu wote waliopo ukumbini hapo watusapoti.

Akaweka pipa stejini pipa hilo lilijaa kupindukia.

Ukiondoa pesa zilizo jaa kwenye Pipa, tulikua tukitunzwa hadi kushangaa.

Kutokana na Show hiyo ndo kwa mara yakwanza Mimi na WERRASON tukanunua Magari.

Mimi nikivinjari na Gari langu aina BMV 320.

12) Ninayo majina mengi kati yamajina hayo nimepewa na Jamaa zangu, kadhalika na Mashabiki wangu.

Bali Jina pekee ambalo nimejipa mwenyewe nilile la MOTOPAMBA likimaanisha jishushe kwenye maisha. Mtu asie na makuu.

Mimi namuamini Mungu ingawa kanisani siendi kila siku.

Sipo hapa kujionyesha ama kuleta mambo ya kinafiki hapana.

Katika maisha yangu sijawahi kwenda kwa mganga au Mtu kuja nipendekeza kwenda kumuona Mganga.

Hua namtanguliza Mungu kwa kila jambo.

13) Wenge mwanzoni uimbaji wetu ulikua kama mchanganyiko wa Orchestra zote za Congo.

Hasa tulikua tukiiga Sebene la ZAIKO, sauti ya Victoria Eleison, Mwenendo na muonekano wa PAPA WEMBA.

kwa mimi binafsi nilikua nikiiga hasa uimbaji wa PAPA WEMBA ambae hua namchukulia kama mfano kwangu.

14) Werrason ni muimbaji mzuri sana wa sauti yapili, nilimkubali zaidi alipochangia kwenye Album yetu ya kwanza ya MULOLO, Wimbo wake NICKY D kauimba kiumaridadi sana.

Binafsi kwenye Album yetu yakwanza nilipenda Wimbo MULOLO.

15) Kwa wale ambao husema kwamba Mimi hua sionekani mchana hadi usiku, nawaelewa bali mimi huanatoka mchana na Watu wangu wa karibu hulijua hilo.

Kwani wakati nikiwa na mualiko kwenye Wizara ya mabo ya nje ntaenda usiku?

Sema siku hizi sipendelei sana kutemebea kwenye Gari kubwa za kifahari maana kuonekana kwangu kwa Umma huleta kizazaa.

16) WENGE tumekaa pamoja tokea Mwaka 1981 hadi 1997 fanyeni mahesabu wenyewe.

Tulikua tukielewana sana, sio urafiki wakawaida bali ndugu.

Kitu kilicho leta mgawanyiko nihasa jambo la kimtazamo.

Mawazo yetu yalikua hayaendani tena sawa.

Na Wapo baadhi ya Watu ambao lengo lau kuu nikuliona Group WENGE limeanguka maana kipindi kile tulikua tupo juu zaidi.

Watu ambao walikua kama ndumia kuwili, wakileta maneno ya uchochezi huku na kule.

Bali Mungu huaga na yakwake, Mgawanyiko umetokea na bado tuliendelea kuwa juu iwe mimi ama Ndugu yangu.

Itaendelea…

Habari Zingine
Tuachie majibu

Anwani yako ya Email haitaonekana