Habari, Utamaduni, Historia na Simulizi za Tanzania na Afrika Mashariki

Riadha kwa Watoto: Tanzania inajiunga na ulimwengu katika kuibua vipaji vya Chipukizi

56

Katika suala zima la kuiba vipaji Kwa watoto programu za kufundisha lazima  ziwe zinnanzia katika msingi au chini Ili kujenga na wanamichezo mahiri watakaofundishwa kitaalamu.

Hapo ndipo suala la ‘Kids Athletics,’ linapoingia.

Kids Athletics ambayp tafsiri yake ni ‘Riadha kwa Watoto,’ ni mafunzo maalum ambayo yameasisiwa na shirikisho la riadha la Dunia (WAF) Kwa lengo la kukuza vipaji Kwa wanamichezo chipukizi kuanzia ngazi ya chini.

Na katika mtaala huu wa michezo, Vijana na Wanafunzi au hasa wanariadha wanaochipukia wanajifunza taaluma mbalimbali isiyopungua 28.

Kozi hii ina lengo la kukuza riadha kupitia maeneo makuu matatu ambayo ni mbio za uwanjani na nyika, kurusha Tufe, Kutupa Mkuki au Javelin pamoja na michezo ya kuruka juu, urefu na pia urukaji wa viunzi.

“Kozi tunaifanya mashuleni sababu pia inakuza uwezo wa udadisi Kwa mwanafunzi, inasaidia kujenga umoja kuhimiza ushindani wa kizalenzo na  kupunguza au kuondoa tatizo la utoro mashuleni,” alisema Charles Maguzu.

Charles Maguzu ni mkufunzi Kutoka Baraza la michezo la Taifa (BMT), kwa upande wa mchezo wa riadha anaetambulika na shirikisho la riadha la Dunia.

Yeye pia ni mtaalamu wa masuala ya elimu kuhusu Kids athletics.

maguzu anaeleza kuwa kozi hiya huweza kusaidia kukuza uwezo wa kuelewa  pamoja kuwajengea vijana uzalendo kuhakikisha wanashiriki michezo, kushinda na uzalendo kwa taifa.

Maguzu anasema mapokeo ya kozi hiyo ni makubwa na kusema anawashukuru wakurugenzi wa halmashauri,wilaya na majiji kote alikopita kwani wamekuwa wakiwaelekeza maafisa michezo wa wilaya kuhakikisha kwamba wanaifuatilia programu hiyo mashuleni ili waalimu waliopata kozi hiyo wakaitafsri kwa vitendo katika shule. 

“Michezo katika nchi yetu imebadilika kuanzia ngazi ya chini hivyotunaamini hao waalimu kwa kutumia Kids athletics wamesababisha chachu ya watoto kupenda michezo iongezeke,  huku tukiona pia vipaji vimeibuliwa kwa wingi”alisema Maguzu.

Alieleza pia amekutana na changamoto kadhaa ikiwemo waalimu asilimia kubwa unakuta ni mwalimu wa michezo lakini hajui mchezo wowote hivyo amekuwa akiwaelimisha maafisa Elimu,wakuu wa shule na wakurugenzi kwa pamoja wahakikishe mwalimu wa michezo awe na taaluma pia amewaomba waalimu wapelekwe kozi za michezo.

“Maeneo mengi ambayo nimepita nimetengeneza waalimu wengi ambao wamekuwa na upeo katika kuanzia kufundisha michezo” alifafanua.

Pia changamoto nyingine vifaa ambapo amewaelekeza waalimu kutumia dhana za kutengeneza ili kufanyia matukio ya kimichezo shuleni na imekuwa inaenda vyema pia baadhi

“Kazi yetu ni kusimamia usajili wa vilabu , kuhakikisha michezo inaendelea katika Taifa letu na kikubwa tunasimamia vyama na mashirikisho kuona namna gani yanafanya kazi kwa kufuata sheria za usimamizi wa michezo katika nchi yetu pia masuala ya utawala bora”.alisema Maguzu..

Safari yake kimichezo hadi kuwa mkufunzi wa Riadha

Charles Maguzu  alimaliza kidato cha nne  mwaka 2001 Bihawana sekondari, mkoani Dodoma, aliendelea na masomo ya kidato cha sita Karatu sekondari 2004 na baada ya kumaliza alienda kuwa mwalimu wa kujitolea.

Mwaka 2005 alijiunga chuo kikuu cha Dar es salaam kwenda kusoma digrii ya kwanza katika masomo ya Physical education sports and culture (Elimu ya viungo pamoja na michezo) hadi mwaka 2008 alipomaliza na kuajiriwa kuwa mkufunzi chuo cha ualimu Mandaka kilichopo Moshi mkoani kilimanjaro.

“Nilifanya kazi kwa muda wa miaka miwili na mwaka 2010 niliajiriwa kuwa ofisa michezo wa wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro baadae  nikapandishwa na kwenda kuwa ofisa michezo mkoa wa Lindi mwaka 2010 hadi 2014” alieleza

Alisema baada ya hapo alihamia mkoani Manyara kuanzia 2014 hadi  2021. ambapo baada us halo alihamishiwa Baraza la michezo laTaifa (BMT) mpaka sasa akiwa mkufunzi na Ofisa .

Michezo kama Taaluma rasmi

Charles Maguzu anaeleza kuwa aliweza kupata Digrii ya michezo na Elimu kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam,.

Piia aliweza kuhudhuria kozi ya kufundisha Kids athletics ambayo iliendeshwa Mwaka 2017 chini ya mkufunzi Hamad Ndee kutoka chuo kikuu  Dar es salaam ambapo tulipewa vyeti watu 12 na kupata maelekezo ya kwenda kuwa wawezeshaji kwenda kufundisha waalimu ili wakafundishe wanafunzi katika shule za Msingi,Sekondari na Vyuo.

“Wakati huo nikiwa Ofisa michezo mkoa wa Manyara nilianza kazi ya kufundisha Kids athletics katika wilaya zote za mkoa wa Manyara nilifundisha waalimu baadae mikoa ya Jirani Arusha, KaratuMwanza, Geuta Lindi, chunya, chato Dar no maeneo mengi nchini” alisema.

Alieleza mpaka sasa kupitia taaluma hiyo ya mkufunzi wa michezo amefanikiwa kufundisha waalimu wasiopungua elfu tatu nchi nzima katika Mikoa 12 na halmashauri 38.

Dar hadi Tokyo

“Mwaka 2021 kupitia programu ya ‘Sports exchanging advisor’nilibahatika kuteuliwa na Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo kupitia baraza la michezo kwenda nchini Japan kufundisha michezo hususani riadha.

Alisema fursa  hiyo aliipata baada yakumliza masomo ya Sports administration na international athletics coaching ambayo alisomea nchini Ujerumani mwaka 2017-2018.

“Wizara ilinipendekeza kwenda Japan ambapo nilikwenda mwezi Septemba 2021 nilisafiri kufanya programu hiyo ya kufundisha riadha,”alieleza.

“Katika nchi ya Japan kwanza nilifundisha Riadha Kids athletics kwa wanafunzi wa Shule za awali hadi msingi, sekondari na wale wanariadha wengine ambao hawakuwa wanafunzi na nilikuwa mmoja wa makocha wa klabu ya Nagai iliyoko Japan,”.

Alisema jukumu jingine alitoa mazoezi ya viungo watu wenye umri mkubwa miaka 60 hadi 110 katika kujenga afya na wawe Imara.

“Jukumu jingine ambalo nililifanya nchini Japan kukuza mahusiano ya kimataifa ilikuwa ni kufundisha mila na desturi za Kitanzania ikiwemo vyakula kuwafundisha lupins pie kuielezea Tanzania ni nchi ya aina gani katika moja ya Radio nchini humo,”aliongeza Maguzu.

Alisema hivi sasa Baraza la michezo kupitia programu yake ya michezo kwa jamii (Sports Community) imeweka mkakati wa kuwa tunatoa mafunzo kwa jamii katika shule,taasisi za Umma na wote wenye uhitaji kupata hiyo taaluma kushirikiana na vyama lengo kuendeleza jamii ipende kushiriki michezo.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari