Taifa Tanzania
Taifa Tanzania. Gazeti Huru la Afrika Mashariki linaloandaliwa kwa lugha ya kiswahili

Historia ya Sanamu la Askari eneo la Samora Jijini Dar-es-Salaam

mnara wa askari, jijini dar es salaam

Historia ya Mnara wa Askari King’s African Rifleman (Askari Bismini) ulio kwenye makutano ya Barabara ya Samora na Mtaa wa Maktaba.

Sanamu hilo ni mmoja ya minara inayofuatiliwa na wadau wa historia Ujerumani. 

Mnara huu ulijengwa mwaka 1920 ukichukua nafasi ya Mnara wa Wissmann maarufu mnara wa Bismin ambao uliwekwa mwaka 1906 kwa heshima ya Meja Hauptmann Hermann von Wissmann.

Wissmann alikuwa kamanda wa Ujerumani (Reichskommissar) ambaye alifanikiwa kukandamiza upinzani kutoka kwa wapiganaji Waafrika katika Afrika Mashariki.

Upinzani wa pwani, hasa ule dhidi ya wakoloni ulioongozwa na Abushiri ibn Salim al-Harthi mfanyabiashara maarufu wa watumwa aliyekuwa mulatto Mswahili-Mwarabu, ulileta changamoto kubwa kwa Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft (DOAG). 

Mnamo tarehe 13 Januari 1889, vikosi vya Abushiri vilichoma moto Kituo cha Misheni cha Benedictine cha Pugu na kuua wamisionari watatu.

Mnara wa Askari Mwaka 1920

Mazingira haya ya upinzani dhidi ya wakoloni yalihitaji kuimarishwa na Ujerumani hivyo katika “kurejesha utulivu na kuanzisha tena ukuu wa Wajerumani” katika pwani ya AfrikaMashariki.

Wissmann alichaguliwa kwa kazi hiyo na Kansela Otto von Bismarck. Kikosi cha Wissmann (Wissmanntruppe) kilikabiliana na Abushiri na kuudhibiti upinzani na hatimae kumfukuza kutoka katika himaya  yake ya pwani na kumlazimisha kupambana na vita vya kujihami ambavyo vilisababisha kukamatwa kwake na hatimaye kuuawa kwa kunyongwa. 

Matokeo yake ni kwamba Dar es Salaam iliokolewa kutoka kwa Waarabu na kwa mara nyingine tena kuondoa unyonge na kukandamizwa kwa wazalendo wanyonge.

Huu ukawa mwanzo wa mwisho kwa vita vya upinzani, kwa amri kutoka Berlin, ilitangazwa rasmi kuwa mji mkuu wa Afrika Mashariki ya Kijerumani (Deutsch-Ostafrika) mnamo Januari 1891, kuchukua nafasi ya mji mkuu wa zamani. 

Mnara wa Wissmann ulikuwa ishara ya serikali ya kikoloni katika Afrika Mashariki ya Kijerumani ambayo iliashiria “taswira ya kikoloni” na kwa hakika ilikuwa eneo linalojulikana sana na wakazi wa Dar es Salaam.

Ingawa Waingereza walibadilisha Mnara wa Wissmann na kuweka Mnara wa Askari baada ya Vita vya Kwanza vya Kidunia, eneo hilo la ukumbusho mahususi na liliendelea kuibua kumbukumbu za Wissmann.

Na pia ikawa Kumbukumbu ya historia ya ukoloni wa Wajerumani kati ya wakaaji wa jiji hilo katika kipindi chote cha utawala wa Uingereza na baada ya uhuru.

Pamoja na matatizo yao, wakoloni walikuwa pia na mema yao machache ambayo yalikinzana na mabaya.

Wissmann alivyofika Afrika Mashariki mbinu aliyotumia kukandamiza upinzani wa Waafrika mwishoni mwa karne ya 19, akichoma mashamba ya chakula, akinyonga yeyote aliyekaidi utawala wa kikoloni.

Na aliweza kuwanyonga hata watemi na machifu ambao walipigwa kitanzi, eneo maarufu pale nyuma ya Kamata.

Pale palikuwepo na mwembe walipigwa vitanzi vya shingo waswahili wengi sana na hapa isisitizwe kuwa Wissmann aliheshimiwa kama shujaa wa kikoloni nyumbani na hata nje ya nchi na hata hapa kwetu.

Hii ni kwa sababu watu walifurahia suala la wa waarabu kupigwa na kushindwaq na wazungu maana na wao walikuwa ni watesi wakubwa dhidi ya watu weusi kwa viwango vyote viovu.

Hivyo basi katika eneo lililotawaliwa na Waingereza la Tanganyika jina lake Wissmann lilienezwa si kwa kusimamisha mnara wake Dar es Salaam tu bali pia kwa kuita mitaa katika miji tofauti baada ya kifo chake.

Mtaa mmoja jijini Dar es Salaam uliitwa Wissmannstrasse, baadaye uliitwa Mtaa wa Windsor sasa unaitwa mtaa wa Azikiwe.

Nadhani Wissmannstrasse ungefaa zaidi kurudishwa kwa heshima yakufuta utumwa kuliko bado tuna mtaa unaitwa Abushiri ambae alishamirisha biashara ya utumwa.