Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Masoud Kipanya aanza maandalizi ya Kufufua Vipindi vya ‘Maisha Plus!’

Mchoraji Maarufu wa Vibonzo nchini, Ali Masoud ambaye hujulikana Zaidi kama Masoud Kipanya ameanza maandalizi ya kuhuisha upya vipindi vya Runinga vya Maisha Plus.

Masoud amerusha katika mitandao mbalimbali safari zake maeneo ya ufukwe wa Bahari ya Hindi na kwingineko ambako ndiko anatarajia kujenga kijiji cha mpito kwa ajili ya washiriki wa vipindi hivyo.

Zamani, ‘Maisha Plus,’ vilikuwa vikirushwa kupitia stesheni ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC).

Bado haijulikani safari hii, Masoud ataamua kutumia chaneli gani.

Ingawa kuna tetesi kwamba huenda akaanzisha channeli yake maalum kwenye mitandao, hususan ‘YouTube.’

Maisha Plus ni shindano maalum la vijana kwa ajili ya kupima uwezo wao wa kustahimili maisha magumu.

Vijana Zaidi ya 30 hupelekwa porini ambako wanatakiwa kujenga nyumba zao wenyewe kisha kuanza maisha humo kwa Zaidi ya wiki mbili wakijishughulisha na ya kilimo, pamoja na mambo mengine mengi ya vijijini.

Katika kijiji cha ‘Maisha Plus,’ hakupatikani huduma za maji wala umeme, pia washiriki hawatakiwi kubeba simu, kompyuta au Televisheni.

Vijana wanaoshiriki ‘Maisha Plus,’ wanatakiwa kujitegemea kwa kila kitu, huku wakizingatia muda maalum wa kazi, kula na kulala.

Maisha yao hurekodiwa moja kwa moja na kamera kuwawezesha watu wengine kuona jinsi vijana hao wanavyoendesha maisha ya ujima, msituni.

Sio wote hufaulu kumaliza siku walizopangiwa kijijini, baadhi huondoka kabla ya muda, ila wanaofika mwisho hupata fungu nono.

Maisha Plus ni wazo linalofanana sana na vile vipindi vya ‘Big Brother Africa,’ vilivyokuwa vinaandaliwa na televisheni ya DSTV.

Masoud, mbali na uchoraji wa vibonzo vya kufikirisha, pia ni msanifu wa picha mbalimbali, mtangazaji, muigizaji na vilecile mvumbuzi wa teknolojia.

Mwaka 2022 alizindua gari lake la umeme lililotengenezwa na kampuni yake ya kaypee motors.

Gari hilo la umeme ambalo linadaiwa kuwa ni wazo binafsi la ubunifu kwa mchoraji huo liliundwa kwa kipindi cha ambalo lilimchukua miezi 11.

Gari hilo lenye uwezo wa kubeba uzito wa kilo 500 linasemekana kuwa ni rafiki kwa mazingira kwa sababu halitumii nishati ya mafuta. Linachajiwa kwa saa sita kabla ya kutumika.

Hata hivyo Zaidi yam waka mmoja tangu kuzinduliwa kwake, gari hilo halijasikika tena.

Kuna taarifa kwamba Masoud alinyimwa vibali vya kuwezesha gari hilo kuzalishwa kwa wingi nchini.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari