Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Waburuzwa Mahakamani Kwa Kuchinja Twiga Mdogo

Wakazi wawili wa kijiji cha Minjingu, wilaya ya Babati mkoa wa Manyara, wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara  kwa tuhuma za kupatikana na nyara za serikali.

Watuhumiwa hao ni Masiali Lais Kipara mwenye umri wa miaka 19 na Paulo Richard (23) ambao pia walikamatwa na silaha tatu aina ya sime pamoja na Mkuki mmoja .

Mwendesha mashitaka wa  Mkaguzi Msaidizi wa polisi, Obedi Machumu mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa Manyara, John Masao alisema, watuhumiwa hao, walikamatwa Februari 14, 2023 saa 11 jioni katika eneo la jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge.

Walikuwa mbioni kumchuna ngozi Twiga mdogo huku tayari wakiwa wamemkata mnyama huyo mguu mmoja.

Twiga huyo anadaiwa kuchinjwa ndani ya eneo la mapito ya wanyamapori la ‘Kwakuchinja!’

Alisema  watuhumiwa hao, walikamatwa na  askari wa wanyamapori, kwa kushirikiana na askari wa Jumuiya ya  hifadhi ya Wanyamapori ya Burunge kwa kushirikiana na Askari wa taasisi ya chem chem.

Alisema watuhumiwa hao, walikutwa na Twiga huyo mdogo mwenye kilo 54.5 ambaye tayari walikuwa wamemuua mwenye thamani y ash 35.1 milioni  mali ya serikali kinyume ya sharia ya umiliki wa nyara za taifa na uhujumu uchumi.

Machumu amesema katikakosa jingine watuhumiwa hao, wamekutwa na sime tatu na mkuki katika mazingira ya kutatanisha ambavyo wametuhmia kufanya uhalifu.

Hata hivyo, watuhumiwa hao, baada ya kuhojiwa na Hakimu, Masao kuhusiana na Mashitaka hayo, Mshitakiwa wa kwanzxa Kipara, alikiri na mshitakiwa wa pili alikana kosa hilo.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Masao, alimtaka Mwendesha mashitaka, Machumu  kuwasomea maelezo ya awali watuhumiwa hao.

Alisema Februari 14, 2011 askari wa wanyamapori  Samweli Daudi  Bayo na James Lesuka na Michael Mbilinyi wakiwa kwenye doria ya kawaida katika eneo  la Burunge WMA, waliwakata watuhumiwa hao, wakiwa na nyama ya Twiga huyo, mdogo wakiwa tayari wamemkata mguu mmoja.

Kipara alikana maelezo hayo na  alieleza mahakama kuwa siku ya tukio yeye alikuwa akiogelewa mtoni na hakuuwa Twiga bali walioua na vijana watu wawili ambao walikimbia ambapo pia alikana kumiliki sime na mkuki.

Mtuhumiwa wa pili pia alikana maelezo siku ya tukio na kueleza alikamatwa akiwa anaelekea nyumbani akitoka kuchunga Ng’ombe.

Mtuhumiwa huyo, pia alikana kumiliki sime na mkuki ambavyo vilikamatwa katika operesheni hiyo.

Baada ya maelezo hayo, upande wa mashitaka ulieleza unba mashahidi sita na  vielelezo vitano na kuomba mahakama ikubali shahido wa kwanza, Sajenti  James (45) kutoa ushahidi wake.

Akitoa ushahidi wake, Sajenti  James alisema mnamo Februari 14, saa 1:30 usiku akiwa kama mtunzaa vielelezo katika kituo cha Polisi Babati alikabidhiwa  nyama ya Twiga, Mkuki na Sime tatu kama vielelezo.

Alisema  vifaa hivyo, alikabidhiwa na afisa Wanyamapori Samweli Bayo kwa ajili ya ushahidi katika shitaka hilo.

Mwendesha mashitaka Machumu, aliomba mahakama kupokea vifaa hivyo kama vielelezo na baadaye aliomba mahakama kuona vyama ya Twiga iliyokamatwa  ili baadaye iteketezwe kutokana na kuanza kuharibika.

Hakimu Masao, alikubaliana na maombi hayo na kutoka nje ya mahakama kushuhudia vielelezo hivyo na baadaye kuagiza kuteketezwa nyama hiyo porini.

Washitakiwa hao, hata hivyo, hawakuwa na pingamizi kuhusiana na kupokelewa vielelezo hivyo na kuteketezwa nyama hiyo.

Hakimu Masao alisema dhamana ya watuhumiwa hao, ipo wazi lakini wanatakiwa kuwa na wadhamini wenye mali ambayo haihamishiki yenye thamani ya zaidi ya milioni 10 namdhamini mmoja mmoja ambao pia watasaini dhamana hiyo.

Kesi hiyo, imeahirishwa hadi Februari 28 na watuhumiwa hao walirudishwa mahabusu ili kukamilisha taratibu za dhamana.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari