Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Safari Kuelekea Mlima Ung’u: Simulizi ya Ujio wa Watu Wanaoishi Meru, Arusha

Twiga wakiwa chini ya kilele cha Ung'u maarufu kama Mlima Meru

Simulizi hii hasa imenukuliwa kutoka kwenye kitabu alichoandika Mathayo Kaaya wa eneo la Akeri mwaka 1907.

Kaaya anaelezea maana ya jina Sakila Kwa kimeru Cha kale kuwa linamaanisha “wapelelezi watazame.”

Hii ni kwa sababu Lamireñ na Kaaya walipumzika Kwa muda katika sehemu iitwayo sakila, wakati wa safari yao ya kwanza.

Maana ya Ngyeku (Kwa Kichaga ni Nkekuu) ni mwanamke aliyezeeka. Au Bi Mkubwa.

Neno Nkanti ambalo ndilo chimbuko la “Kikatiti,” ni mwanamke bado hajazeeka au mke mdogo.

Sasa basi Lamireñ alivipa vile vilima majina yake Kwa heshima ya wake zake wawili.

Lamireñ na Kaaya baada ya muda, wakaondoka kuelekea Ung’u au Mlima Meru.

Lamireñ akaishi kwenye pango na watu wake, huku Kaaya akiondoka kuelekea upande wa magharibi hadi sehemu alipopaita Midawe.

Hawa ndo wanadaiwa kuwa ndio watu wa kwanza kabisa kufika katika eneo lililo chini ya Mlima Meru, Kilele ambacho wao walikiita Ung’u.

Lamireni na Kaaya walitokea Milima ya Usambara, ambako kwa sasa ni Mkoani Tanga.

Hata hivyo, Usambara hapakuwa nyumbani kwao, pale walifanya kupumzika tu.

Sasa inasemekana kuwa ile jamii ya wasambaa waliyoikuta maeneo yale iliamini sana mambo ya kishirikina.

Basi, kwa kuhofia ushirikina waliamua kuondoka kule Usambara mapema katika safari ambayo hayimaye iliwafikisha chini ya Mlima Meru, kilele cha pili kwa urefu nchini Tanzania baada ya Kilimanjaro.

Baada ya kufika kwa Lamiren na Kaaya chini ya Mlima Meru, jamii zingine ziliendelea kuja katika eneo hilo.

Watu waliofuata walikuwa wanakuja kwa makundi makundi katika nyakati tofauti.

Walipofika eneo Ung’u (mlima Meru) waliwakuta jamii ya wakoningo, watu ambao baada ya kuona wageni wanafika kwa wingi maeneo yao wao waliamua kuhama.

Kuna taarifa zinazodai kuwa Wakoningo walikimbilia upande wa magharibi mbali zaidi hadi kuifikia misitu ya kama congo.

Hii ni historia kutoka kwa wazee wa eneo la Meru. Wazee Hawa karibia wote wamesimulia nadharia inayofanana, hivyo kuthibitisha matukio yote kuwa ni sahihi kabisa.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari