Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Wananchi 200 wanufaika na kambi maalum ya matibabu ya Mifupa Sumbawanga

Zaidi ya wananchi 200 wa Mkoa wa Rukwa na mikoa ya jirani wamepatiwa huduma za uchunguzi na matibabu ya  mifupa katika kambi ya maalum ya tiba ya upasuaji kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga.

Shughuli hizo za siku tano ziliratibiwa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Kiongozi wa Kambi hiyo  Dk Baraka Mponda, kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya amesema mwitikio ulikuwa mkubwa.

“Wananchi wengi walijitokeza kupatiwa za matibabu na hivyo basi hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya itaendelea kusogeza huduma zake za karibu na jamii za Nyanda za Juu Kusini,” aliongeza.

“Tumehudumia wagonjwa zaidi ya 200, ambao kati yao wagonjwa 12 walilazwa na kupatiwa huduma za matibabu ya upasuaji mkubwa wa mifupa, na wengine tuliwapa matibabu na kuwaruhusu. Wagonjwa wengi tuliowaona walikuwa wamepata ajali na kuumia na wengine walijaribu hata kwenda kupata matibabu yasio rasmi kwa waganga wa kienyeji!”

Uwepo wa kambi hiyo imesaidia kuwapunguzia gharama za usafiri na malazi kwa wananchi kufuata matibabu hayo jijini mbeya, vilevile kubadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo wataalamu wa hospitali ya rufaa ya mkoa sumbawanga kwenye kutoa matibabu kwa wagonjwa wa mifupa na ajali.

Mponda ameishauri jamii kuacha kupelekwa wagonjwa wa ajali na mifupa kwa waganga wa kienyeji kwasababu wanamcheleweshea mgonjwa kubata tiba sahihi na kusababisha magonjwa kupelekwa hospitali wakati tatizo limeshakuwa kubwa.

Vilevile amewataka watumiaji vyombo vya moto kuwa waangalifu na kufuata uweledi wa kuvitumia kwani ajali nyingi zinazotokea zinasababisha watu kupoteza viungo na wengine kuwa na ulemavu  wa kudumu unaotokana na uzembe wa waendesha vyombo vya moto.

Nae Raheli Nkya Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga ameushukuru Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya  kwa kuratibu na kuwezesha ufanyikaji wa kambi hiyo kutokana na mahusiano mazuri na kutaka huduma hizo ziendelee kufanyika mara kwa mara.

“Tunawapongeza Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kutuletea Madaktari Bingwa nami nimejifunza kutoka kwa madakta namna ya kumshauri na kuhudumia kutoka na matatizo mgonjwa aliyonayo!”

Octavian Kipengele ambaye ni Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga ameuomba Uongozi wa hospitali ya kanda kuendelea kuleta huduma za mkoba kwa matibabu ya mifupa kutoka na kukosekana kwa huduma za kibingwa katika mkoa huo ambao unasababisha wananchi kupewa rufaa kwenda jijini mbeya kufwata matibabu hayo.

Godfrey Constantine, Fanuel Simsonga na Yusta Matofali ni miongoni mwa wananchi waliojitokeza kupatwa huduma katika kambi hiyo ya matibabu, wameeleza jinsi gani ujio mwa madadktari bingwa katika Mkoa wa Rukwa umekua ni wa manufaa kwao baada ya kupatiwa matibabu na hali zao kuendelea kuimarika vyema.

Kambi ya matibabu ya mifupa iliyoratibiwa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imefanyika kwa siku 5 mkoani Rukwa katika hospitali ya mkoa Sumbawanga

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari