Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Waalimu Tanzania ndio wahanga wakubwa wa Mikopo laghai maarufu kama ‘Kausha Damu!’

Benki ya NMB imeanza mpango maalum wa kuwafikia waalimu wote Tanzania kupitia makongamano maalum ya ‘Siku ya Waalimu,’ yatakayoandaliwa na benki hiyo katika mikoa 17 nchini mwaka huu.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa biashara kwa wateja wadogo na wa kati, Martine Masawe, lengo la benki hiyo ni kukutana na waalimu Zaidi ya 9000 kupitia mikutano 30 itakayofanyika nchini.

“Tumedhamiria kutoa elimu kwa waalimu nchini na vile vile kuwaokoa kutokana na mikopo ya mitaani, maarufu kama kausha damu ambayo imekuwa ikimaliza mishahara yao,” alifafanua Masawe.

Akizungumza katika siku wa waalimu (Walimu Day), mkoani Arusha, Afisa Biashara huyo amesema Benki ya NMB imepunguza riba za mikopo kwa waalimu hadi kufikia aslimia 9 tu.

Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus amesema kuwa zaidi ya waalimu 200 wamehudhuria kungamano la kwanza la ‘Walimu Day,’ kwa mwaka huu, lililofanyika jijini Arusha.

“Mikutano kama hii imekuwa ikifanyika kwa miaka tisa sasa na ilizinduliwa rasmi huku kwenye kanda ya kaskazini, mjini Korogwe, Tanga,” Ladislaus alifafanua.

Kwa mujibu wa Meneja wa Kanda, NMB sasa inafanya juhudi kuhakikisha waalimu, pamoja na wateja wengine wa benki hiyo wanatumia huduma zao mpya za kidijitali ili kurahisisha kutoa na kupokea fedha kwa usalama na haraka.

Akifungua siku hiyo maalum ya waalimu Mkoani Arusha, Afisa Elimu Taaluma Shirley Sway ameisifu benki ya NMB kwa kuja na mkakati wa kuwasaidia waalimu kupata mikofo yenye masharti nafuu na riba ndogo.

“Hii mikopo ya vikundi vya mitaani imkuwa ni tatizo kubwa nchini hasa kwa waalimu kiasi kwamba wakati mwingine huwa tunalazimika kuita polisi ili kuwadhibiti watu wanaowafuata walimu hadi majumbani, wakati mwingine hata shuleni wakifundisha kuwadai pesa,” alisema.

Imeelezwa pia katika mkutano huo kwamba asilimia 80 ya wateja wa benki ya NMB nchini, ni waalimu, hivyo taasisi hiyo ya fedha inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kundi hilo linahudumiwa vizuri na pia kulindwa ipasavyo.

Hadi sasa idadi ya waalimu nchini imefikia 250,000 huku watu wa taaluma hii wakiendelea kuongezeka.–

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari