Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Maabara kubwa ya kupima Ubora wa Mbegu za kilimo kwa teknolojia ya kisasa kujengwa Morogoro

TAASISI ya Udhibiti ubora wa mbegu Tanzania iko mbioni kujenga maabara mpya, kubwa na ya kisasa zaidi kwa ajili ya kuchambua, kupima na kukagua mbegu kabla hazijapewa ithibati.

Mkurungezi Mkuu wa taasisi hiyo (TOSCI), Patrick Ngwediagi amesema maabara hiyo mpya itakayotumia teknolojia mpya ya kidijitali, inajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 980, mkoani Morogoro, ambako ndiko yaliko makao makuu ya taasisi hiyo.

Wakati huo huo taasisi hiyo imewataka wakulima na jamii kwa ujumla kuacha matumizi holela ya mbegu na badala yake watumie ambazo zimethibitishwa ubora ili kuongeza mavuno, tija na kipato.

Kwa mujibu wa Dk Ngweadiagi, ili kilimo kuwa na tija nchini wakulima wanapaswa kutumia mbegu zenye ubora na zilizothibitishwa na taasisi hiyo ili kuongeza mavuno na kipato.

“Wito wangu kwa wakulima na jamii kwa ujumla tumieni mbegu zilizothibitishwa ubora ili kuongeza mavuno,tija na kipato badala ya kuendelea kutumia mbegu ambazo hazina ubora na kupunguza tija kwenye kilimo nchini” alisema 

Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 alisema watatumia kiasi cha Sh.bilioni 12.6 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali.

Alisema moja shughuli watakayoifanya ni kuendelea na uboreshaji wa shughuli za utafiti na usimamizi wa ubora wa mbegu.

“Taasisi itaendelea kuboresha shughuli za uthibiti na usimamizi wa ubora wa mbegu zilizoanzishwa katika mwaka wa fedha uliopita katika maeneo mbalimbali”alisema

Kadhalika, alisema shughuli nyingine ni kutekeleza mradi wa kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi (AFDB) kwa kujenga maabara yenye uwezo mkubwa.

“Maabara hii itawezesha taasisi kufanya uchambuzi wa mambo mbalimbali yanayohusu mbegu katika makao makuu ya TOSCI”alisema

Aidha, alisema pia wamepanga kujenga maabara ya mbegu kwenye tawi la taasisi hiyo kanda ya ziwa mkoani Mwanza .

“Pia kuandaa na kutekeleza mkakati wa kuelimisha umma juu ya matumizi ya mbegu zilizothibitishwa ubora za zenye  lebo ya TOSCI.

“Kuthibitisha na kusimamia  ubora wa miche na vipando na pingili za mazao ya miti ya matunda,migomba na miwa”alisema

Hata hivyo, alisema katika kipindi cha miaka mitano ilihopita taasisi hiyo imesajili zaidi ya mbegu 647 na kuwachukulia hatua watu wote waliobainika kuuza mbegu feki kwa kuwafikisha mahakamani.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari