Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Zaidi ya watu 40,000 hupata Saratani kila mwaka

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwajulia hali wagonjwa Mkoani Geita (Maktaba)

Kansa na magonjwa mengine mageni yasiyo ya kuambukizwa yanaendelea kuwa tatizo kubwa nchini Tanzania.

Wizara ya afya kupitia kitengo cha magonjwa yasiyoambukiza nchini imewatahadharisha watanzania juu ya kuacha mtindo mbovu wa Maisha kwani inaongeza Visa vya magonjwa yasiyoambukiza.

Mitindo mibovu wa Maisha Ni pamoja na unywaji wa pombe Kali kupita kiasi, matumizi ya sigara na madawa ambayo yamekuwa visabaishi vya magonjwa yasiyoambukiza.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi msaidizi wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka wizara ya afya, James Kiologwe katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa sekta ya afya jinsi ya kutibu magonjwa yasiyoambukiza.

Alisema kuwa zaidi ya watanzania million tano ambayo ni sawa na asilimia 26 Wana shinikizo la juu la damu, na wengine milioni moja wanaugua kisukari huku Visa zaidi ya 40, 000  vya magonjwa ya saratani yakitokea kila mwaka. 

“Haya yote yanatokana na mtindo m’bovu wa Maisha na matibabu yake yanagharimu zaidi ya Trillion 2.8 ambayo tungechukua tahadhari fedha hizi zingefanya Mambo mengine”

Aliwataka watumishi hao kwenda kutoa elimu kuanzia ngazi ya jamii juu ya tahadhari ya kujikinga na magonjwa haya lakini wawe makini zaidi ya mafunzo wajue namna sahihi ya kuyatibu ili kuokoa nguvu kazi ya Taifa inayopotea kila mwaka kutokana na magonjwa haya.  

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na wizara ya afya kwa kushirikiana na ofisi ya Rais Tamisemi, iko katika kutekeleza mpango mkakati maalum kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza ambayo wanalenga kuwafikia watumishi 2632 Hadi kufikia desemba 2023.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya siku tano, meneja mpango wa mradi wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka wizara ya afya, Valelia Milinga alisema mpango huo unatekelezwa kwa kuzingatia vipaumbele vya sekta ya afya.

“Mpango huu unaolenga kuimarisha mfumo wa utoaji huduma za afya kwa Kinga na tiba za magonjwa hayo kuanzia ngazi ya jamii hadi Taifa ambapo leo watumishi 360 wananufaika na mafunzo haya ya awamu ya tatu”

Alisema moja ya mkakati ni kuimarisha huduma za msingi kwa kuzijengea uwezo vituo 600 vya afya nchini kwa kuzingatia kila kituo kiwe na muhudum angalau mmoja. 

Akifungua mafunzo hayo, mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela aliwataka watumishi hao kuzingatia mafunzo ili kuweza kutoa elimu kwa jamii jinsi ya kujikinga na magonjwa na Kinga ili kupunguza Visa vipya lakini vifo pia.

Mongela aliyewakilishwa na mganga mkuu wa mkoa Dr. Silvia Mamkwe aliwataka watumishi hao kuwa na utaratibu wa kuandaa ripoti ya wagonjwa wao kila miezi mitatu ili kurahisisha mapambano ya magonjwa hayo kwa kuwa na data halisi.

Habari Zingine
Tuachie majibu

Anwani yako ya Email haitaonekana