Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Mbulu Mbioni Kurejesha Sifa yake kwenye Riadha za Kimataifa

HALMASHAURI ya mji wa Mbulu sasa imeamua kurudisha sifa ya wilaya hiyo katika kuwaibua wanariadha wa kimataifa.

Mbulu tayari imeanza taratibu mpya za kimichezo hususan mbio za nyika katika mpango wake wa kuwatengeneza wanariadha wapya watakaokuwa Nyota nchini na katika viwanja vya kimataifa.

Afisa Michezo wa halmashauri ya mji wa Mbulu, Benson Maneno anasema wameamua kuinyanyua Mbulu kimichezo hasa kupitia riadha kwa kuanzisha kituo cha kukuza na kuwaendeleza wakimbiaji chipukizi.

Kituo hicho kipya cha kuwatengeneza wakimbiaji wa kimataifa kinajulikana kama ‘Mbulu town council Athletic Club’.

Maneno anaongeza kuwa ofisi yake ina mipango ya muda mfupi na mrefu katika kutafuta, kuwafundisha na kuwatengeneza Wanariadha Nyota watakoipeperusha vyema bendera ta Tanzania kimataifa.

Hivi karibuni wanariadha vijana kutoka Mbuli walishiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano ya vijana ya riadha, jijini Arusha, kuonesha kuwa tayari kituo chao imeanza kuzalisha wanamichezo bora.

Katika Mashindano hayo ya riadha ya Vijana (TAYAC) yaliyofanyika mkoani Arusha, Mbulu iliweza kushika nafasi ya tatu, pamoja na kwamba hii ni mara yake ya kwanza.

“Tulishiriki kwa mara ya kwanza na tukashika nafasi ya tatu. Tulifanikiwa kutwaa medali kadhaa na kwetu huo ulikuwa ni ushindi wa kishindo,”alisema Maneno.

Inaonekana pia uwa katika mashindano hayo ya vijana, Mbulu iliwakilishwa na wanariadha wanariadha wachache.

Hata hivyo, tayari wamerudi kambini kuanza upya mazoezi kwa ajili ya mashindano kama hayo mwakani TAYAC 2023.

Kwa miaka mingi huko nyuma, Mbulu ilikuwa ndio chemchemi ya riadha na chimbuko la wakimbiaji wakubwa nchini.

Hata hivyo wilaya hiyo baadae ilianguka kimichezo na sasa viongozi wameamua kuifufua tena.

Kituo cha Michezo mjini Mbulu kwa sasa kinafundisha vijana 15, huku usajili wa wanamichezo wengine wachanga ukiendelea.

“Mpango huu umelenga medali zote ambazo zinatafutwa Tanzania ziwe zinatokea Mbulu kupitia wakimbiaji watakaokuwa wameandaliwa vyema kutokea katika kituo chetu,” anaahidi Benson Maneno.

Alisema klabu hiyo itakuwa ikishiriki mashindano mbalimbali yakiwemo ya kitaifa na kimataifa na kuongeza kuwa watashirikiana na wadau wengine wa Riadha kuhakikisha mpango huo unafikia malengo yaliyokusudiwa.

Mmoja wa  wanariadha mashuhuri anayetokea Wilayani Mbulu ambaye kama taifa linakumbuka mchango wake katika kuipeperusha bendera ya Tanzania ni mwanariadha John Steven Akwari ambaye moja ya mashindano aliyoshiriki ni michezo ya Olimpiki mwaka 1968, nchini Mexico.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari