Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Mjusi Yesu Mwenye Sifa ya Kutembea Juu ya Maji

Duniani kuna MJUSI  anaetembea juu ya maji kwa miguu miwili.

Mjusi huyu kitaalamu anaitwa BASILISCUS. Kwa kiswahili hujulikana zaidi kama MJUSI YESU,

Ameitwa jina hilo kwasababu Yesu kwa mujibu wa bibilia alikua na uwezo wa kutembea juu ya maji,

Mjusi huyu anapatikana katika bara la Amerika ya Kaskazini na Amerika ya Kusini.

Anapenda kuishi pembezoni mwa mito na katika mapori makubwa yanayopatikana katika nchi zilizomo katika mabara hayo mawili.

Mjusi huyu ana rangi ya kahawia na krimu. Pia amejaaliwa kuwa na mdomo mkubwa.

Madume ya mijusi hii huwa na vifua vipana zaidi kuliko majike.

Urefu wa Mjusi Yesu kutoka mkiani hadi kichwani ni takriban sentimita 76 ambazo ni karibu futi 2.5. 

Jike la Mjusi huyu anaweza kufikia uzito wa hadi gramu194. 

Ajabu ni kuwa mkia wa mjusi huyu unachukua karibu asilimia 75 ya mwili wake wote.

Basiliscus huyu ana uwezo wa kukimbia kilometa 1 kwa saa anapokuwa juu ya maji.

Licha ya  kutembea juu ya maji, yeye pia ni hodari sana katika kuogelea na kupanda miti.

 Kiumbe huyu ana uwezo wa kuzama chini ya maji na akatulia kwa muda wa hadi nusu saa. 

Umri wao wa kuishi ni miaka saba ila umri huu ni kwa wale wa kufugwa. 

Kwa upande wa wale wa porini umri wa kuishi ni mdogo zaidi, kutokana na hatari wanayokumbana nayo ya kushambuliwa na kuliwa na viumbe wengine.

Chakula, Uzazi na Maadui wa Mjusi Yesu

Mjusi basiliscus hula wadudu wadogo akiwemo bilimbisa kimba (bittle). 

Pia mijusi hawa wanakula minyoo, maua, inzi, mayai na samaki wadogo.

Kwa upande wa uzazi, mijusi basiliscus wanataga mayai kati ya 10 na 20. 

Mijusi hawa hutaga mayai kwa mafungu mafungu Sehemu btofauti,

Hii ina maana, kama atataga mayai 20, hatagi maya hayo yote muda mmoja.

Anaweza kutaga mayai manne au matano, kisha akataga sehemu nyingine mayai matano au zaidi …hivyo hivyo… mpaka anafikisha 20.

Maadui wakubwa wa mjusi huyu ni ndege aina ya tai na baadhi ya wanyama.

Mjusi huyu anaweza kutembea kwenye maji na nchi kavu lakini akitembea juu ya maji anatumia miguu ya nyuma.

Miguu ya mjusi basiliscus ni mipana na  chini ya miguu hiyo kuna vitu fulani kama sponji ambavyo vinatoa povu. 

Hali hiyo ya miguu yao ndiyo inayowafanya wasizame wanapotembea juu ya maji.

Wanapokuwa wadogo wanaweza kwenda umbali mrefu zaidi juu ya maji kuliko wanapokuwa wakubwa. 

Mjusi basiliscus mdogo anaweza kukimbia umbali wa hadi wa kilomita 20 kwenye maji,

Licha ya kuishi ndani ya maji mjusi basiliscus anaweza pia kuishi ardhini ambako ndiko hasa kwenye makazi yake ya kudumu. 

Mjusi basiliscus ana tabia pia ya kujificha chini ya majani kukwepa adui zake.

Mjusi huyu ni bingwa wa kujificha anapoona adui. Anapokuwa nje ya maji anaweza kujituliza sehemu kwa muda mrefu bila hata kutikisika sehemu yoyote ya mwili wake.

Habari Zingine
Tuachie majibu

Anwani yako ya Email haitaonekana