Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Mwembe wa Ikulu Kutimiza Miongo 60 ifikapo Mwaka 2024

Pale katika Jengo la Ikulu iliyopo jijini Dar-es-salaam kuna mti mkubwa wa Mwembe.

Sio wengi wanajua historia ya mti huo ambao utatimiza miaka 60 ifikapo mwezi wa Nnne wa Mwaka 2024.

Mtaalamu wa historia, Abbas Mwalimu anaeleza kuwa mti huo wa mwembe uliopo katika viwanja vya Ikulu ya  Magogoni jijini Dar es Salaam ulipandwa tarehe 26 Aprili 1964.

Kuoteshwa kwa mti huo ilikuwa ni moja ya matukio maalum la ishara ya kumbukumbu baada ya tukio la kuchanganywa kwa udongo wa upande wa bara, enzi hizo Tanganyika, na Visiwani, yaani Zanzibar.

Mmoja kati ya watu waliobeba udongo wa Zanzibar na kuchanganywa na ule wa Tanganyika, ni Hassan Omar Mzee kutoka Unguja.

Udongo kutoka pande mbili za nchi ya Tanzania zilizotenganishwa na bahari ya hindi, lilifanyika katika Uwanja wa Uhuru mwaka 1964.

Wengine walioubeba udongo uliochanganywa kutoka pande mbili za Muungano ni Hassan Kheir Mrema na Sifaeli Kunda kutoka iliyokuwa Tanganyika na Khadija Abbas kutoka Zanzibar.

Sifaeli Shuma aliyekuja kuwa Mwalimu wa sekondari na baadae kuwa mkuu wa shule ya Machame Girls, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

Siku hiyo pale Ikulu ya Dar-es-salaam pia kulifanyika tukio kubwa la kihistoria la kupandwa mti wa mwembe kwa ajili ya kumbukumbu ya Muungano.

Mwembe huo ulipandwa na Mwalimu Julius Nyerere akishirikiana Mzee Abeid Amani Karume.

Mti huo ulipewa jina la ‘Mwembe wa Muungano.’

Udongo uliobakia na vifaa vilivyotumika katika shughuli nzima vilipelekwa kutunzwa ndani ya Makumbusho ya Taifa.

Udongo wa Zanzibar uliochanganywa na ule wa Tanganyika ulichimbwa kutoka eneo la Kizimbani Unguja.

Kwa upande wa Tanganyika udongo ulichotwa kutoka jijini Dar es Salaam.

Muungano wa Tanganyika na Visiwa vya Unguja na Pemba pia utatimiza miaka 60 mwezi wa nne mwaka 2024.

Sasa huo dio mti wa mwembe uliopandwa kama alama ya kudhihirisha Muungano wa pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tukio hilo likifanyika kwa ajili ya kuusimika zaidi udugu wa kudumu wa wakazi wa bara na visiwani ambao inadaiwa kuwa walikuwa na mahusiano ya karibu yaliyoanza karne nyingi zilizopita.

Hivyo basi mwembe unaoonekana katika viwanja vya Ikulu ya Dar es Salaam ulioteshwa na hatimaye kumea juu ya kifusi cha udongo uliochanganywa kutoka pande mbili za Muungano, yaani Bara na Visiwani.

Kwa sasa unaitwa tu “Mwembe Muungano.” Kama jina rasmi ingawa wengine hupenda kusema ni ‘Mwembe wa Ikulu.’

Awali kabla ya historia hii ya mti kuanzania kusahaulika, baadhi ya watafiti wa Mambo wamekuwa wakiuita mwembe huo kuwa ni “Mwembe wa Tanzania!”

Ikumbukwe kuwa maeneo yenye jina la miti ya miembe sio mageni nchini na hata nchi jirani.

Jijini Dar-es-salaam kuna eneo linaitwa ‘Mwembe Chai.’

Mkoani Kigoma kuna eneo jingine ambalo nalo linaitwa ‘Mwembe Togwa!’

Mwembetogwa pia ni jina la kata ndani ya Mji wa Makambako katika Mkoa wa Njombe, Nyanda za juu Kusini mwa Tanzania. Wakati wa wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, Mwembetogwa ilikuwa na wakazi wapatao 7,382.

Katika mji wa Mombasa, nchi jirani ya Kenya nako utakuta eneo linaloitwa Mwembe Tayari.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari