Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Abiria wa Ndege kati ya Songea na Dar-es-Salaam waongezeka kila siku

Idadi ya wasafiri wa ndege Dar-Songea yaongezeka

Idadi ya abiria wanaosafiri kwa ndege za umma kati ya Mkoa wa Ruvuma, ulioko kusini mwa Tanzania na Dar-es-salaam inaelezewa kuongezeka kila kukicha.

Hatua hii inaonesha kuwa uwanja wa ndege wa mjini Songea, Mkoani Ruvuma sasa umeanza kuwa na shughulki nyingi na muda wowote unaweza kuhitaji ndege nyingine ya pili kuwahudumia wasafiri wanaoongezeka. 

Meneja wa Uwanja wa Ndege Songea Jordan Mchami amesema idadi ya abiria wanaosafiri kwa ndege ya Air Tanzania kutoka Songea kwenda Dar-es-salaam imekuwa kubwa kiasi kwamba kuna wakati viti vyote hujaa kabisa.

Mchami amefafanua kuwa wasafiri hao wameongezeka hadi imekuwa kwamba ndege ta ATC yenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila inapofika Songea, huwa inarudi tena Dar-es-Salaam ikiwa na idadi hiyi hiyi ya wasafiri.

Zamani ndege kutoka Dar ikiwa na abiria 76 ilikuwa inaweza kurudi na watu wachache sana.

Hivi sasa idadi ya wasafiri kutoka Ruvuma ikipungua, kwa mujibu wa taarifa za uwanjani hapo, pengine abiria wawe 70 lakini sio chini ya hapo.

Usafiri kati ya Sengea na Dar-es-salaam mara nyingi hufanyika kwa mabasi, huku kampuni ya Super Feo ikionesha kutawala ruti hiyo.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari