Taifa Tanzania
Taifa Tanzania. Gazeti Huru la Afrika Mashariki linaloandaliwa kwa lugha ya kiswahili

Idadi ya Watanzania Sasa Imefikia Milioni 61.741

Idadi ya watanzania imeongezeka

Taarifa rasmi ya sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022, inaonesha kuwa kuna jumla ya Watanzania 61,741,120.

Naam. Watu Millioni 61.7 ni idadi inayokimbilia Milioni 62. Sasa kati ya wananchi wote wa Tanzania waliohesabiwa, wanawake wameendelea kuwa wengi zaidi idadi yao ikiwa ni zaidi ya asilimia 51 ya watu wote nchini.

Kuna jumla ya wanawake 31,687,990 nchini Tanzania, kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya kitaifa ya watu na makazi kwa mwaka 2022, yaliyotangazwa rasmi jijini Dodoma na Rais Samia Suluhu Hassan.

Wakati huo huho jiji la Dar-es-salaam ndilo lenye idadi kubwa zaidi ya wakazi nchini.

Idadi ya watu wanaoishi katika mkoa wa Dar-es-salaam ni 5,383, 728 ambayo ni sawa na asilimia 8.7 ya watu wote nchini.

Mwanza ni mkoa wa pili kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu, ukiwa na wakazi wapatao Milioni 3.7.

Visiwa vya Zanzibar, yaani Unguja na Pemba hadi sasa vina jumla ya watu takriban Milioni 1.9.

Wakati huo huo sensa ya watu na makazi nchini imebaini uwepo wa majengo Millioni 14.4 kote nchini.

Kati ya majengoi hayo, majengo 440,421 yako visiwani Zanzibar.

Sensa ya Kitaifa ya watu na makazi nchini Tanzania, hufanyika kila baada ya miaka 10.