Habari, Utamaduni, Historia na Simulizi za Tanzania na Afrika Mashariki

Hatimaye Wahadzabe Sasa Waanza Kusoma Hadi Sekondari

Wahadzabe wakirejea katika makazi yao pangoni, wakitokea mawindoni

Jamii ya Wahadzabe ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi porini bila kuwa na msukumo wowote wa kupata elimu rasmi, sasa wameanza kujiunga na shule za msingi pamoja na sekondari.

Wahadzabe hao ambao wanaishi katika Tarafa ya Eyasi na Endabash wilayani Karatu, wamewezeshwa kupata elimu muhimu kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii, yaani TASAF. 

Mara nyingi, jamii ya wahadzabe ambayo ina watu wachache zaidi nchini, imekuwa ikiishi kwa kutegemea uwindaji wa wanyama pori, uchimbaji mizizi pamoja na kuchuma matunda ya porini kama vyakula vyao vikuu.

Na kwa sababu vyakula hivyo hupatikana kirahisi katika maeneo yao, wengi hawakuona sababu au umuhimu wa kuishi maisha ya aina nyingine, ikiwemo kulazimika kuhudhuria elimu za mashuleni.

Baadhio ya wahadzabe kutoka Kijiji Cha Endamaghan ambao ni wanufaika wa mfuko wa maendeleo  ya jamii pamoja na ruzuku wanazozipata kutoka TASAF wanasema taratibu wengi wao wameanza kuona umuhimu wa elimu.

Na wanakiri kuwa fedha wanazopata kutokana na mpango wa kunusuru kaya masikini nchini pia zinawasaidia kubadilkisha maisha yao ya kizamani waliyokuwa wanaishi tangu zama za watu wa mawe.

Msemaji wa jamii  hiyo kutoka kituo Cha Ushindi, Dalali Julius amesema TASAF imewezesha jamii hiyo ambayo ilikuwa haijui Elimu ya juu zaidi ya darasa la Saba kujiongeza kidogo.

Awali hapakuwa na watoto wa Kihadzabe katika shule za sekondari lakini sasa kuna wanafunzi kutoka jamii hiyo wanaosoma hadi kidato cha nne na baadhi wamenza kujiunga na vyuo.

Inadaiwa kuwa ni Mhadzabe mmoja tu nchini aliyewai kufika chuo kikuu ingawa taarif zake hazikuweza kupatikana mara moja.

Dalaly aanabainisha kuwa kwa sasa jamii hiyo imneanza kufanya shughuli za kiuchumi ikiwemo ufugaji wa nyuki, mradi waliouanzisha mwaka 2019 baada ya kupewa mizinga 30 kutoka mfuko wa maendeleo ya jamii.

Aliendelea kueleza kuwa mizinga hiyo kwa Sasa ndiyo inayowasaidia jamii hiyo kwa kuwasomesha wanafunzi zaidi ya Tisa wanaosoma shule mbalimbali za secondary zilizoko wilayani Karatu na nje ya wilaya.

Dalaly ambaye ndiye msemaji wa jamii hiyo alisema kuwa kwenda shule za upili kwa jamii hiyo ni muujiza kwani kabla ya TASAF wamekuwa wakiishia darasa la Saba

Huku ukame ukiathiri maeneo mengi nchini, wahadzabe wamekuwa wakiteseka kwa sababu vyakula vuao vinavyotegemea zaidi mazingira asili vimeanza kutoweka.

Hata hivyo kutokana na miradi yao ya uchumi wengi sasa wanaweza kununua chakula, mbali na matunda mwitu au uwindaji.

“Zamani sisi hatukujua maana ya Milo mitatu. Kawaida asubuhi tukiamka mtu akiona hamna kitu cha kula basi angeondoka kwenda porini kutafuta chochote,” alisema Dalali.

“Ni tofauti na jamii zingine ambazo watu wao huanza siku na kifungua kinywa lakini hicho kwetu hakipo,” aliongeza Dalali.

Alisema kwa Sasa mizinga hiyo imewaletea matunda makubwa ambapo wanapata asali kilo 20 Hadi 60 Kila baada ya miezi mitatu au minne na huwa wanauza kilo moja ya asali kwa shilingi elfu moja (1000).

Ambapo wanufaika walikaa na kupitisha fedha hizo zitumike kwenye huduma ya Afya na Elimu ikiwemo kuwapatia mahitaji wanafunzi na pia kulipa bili kwa ajili ya matibabu ya walengwa.

“Pamoja na kuwalipia wanafunzi mahitaji ya shule na ada pia wamejiwekea utaratibu katika zahanati ya Delmondo kulipa matibabu ya walengwa kwa bili Kila wakipata chochote wakiuza asali.”

Jamii hiyo kwa pamoja wameishuru serikali kwa mpango huu na kuomba kuongezewa mizinga kwani bado mahitaji ni makubwa kwa jamii na fedha wanazozipata ni kidogo haitoshelezi.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari