Habari, Makala na Simulizi kutoka Afrika

Tanzania na Mawe kutoka Sayari za Mbali

Kimondo kikishuka duniani kutoka anga za mbali

Tanzania Ni nchi ambayo ipo upande wa mashariki wa bara la Afrika.

Kwa lugha nyingine nchi ya Tanzania imo ndani ya Dunia, sayari ambayo ipo katika mfumo wa nyota inayoitwa Jua au solar system na pia ndani ya kundi jumuishi la nyota, yaani milk way

Tanzania Ni moja Kati ya nchi chache duniani ambazo zimeangukiwa na vimondo.

Na nchi ina ushahidi wa uwepo wa vimondo au vipande vya vimondo kikiwemo kile kilichotua katika wilaya ya mbozi, Songwe (Sasa liko chini ya uangalizi wa Mamlaka ya Ngorongoro).

Jiwe jingine ni lile lililotua eneo la kwimba huko Malampaka, mkoani Shinyanga.

Pia kuna taarifa ya uwepo wa kimondo wilayani Karatu, mkoani Arusha. Kimondo kinachodaiwa kushuka mwaka 1911 na kumezwa kabisa ndani ya ardhi

Kuangukia kwa vimondo hivi katika nchi ya Tanzania sio suala lililofanyiwa utafiti mkubwa.

Na tangu miaka hiyo mingi ya kushuka kwa vipande hivyo vya mawe ya madini kutoka anga za nje, wakazi wa maeneo husika bado wanajiuliza hivyo ni vitu gani.

Kimondo cha Songwe

“Hili Ni jiwe gani? Je, lina tofauti na yale mengine ya ardhini?

Pale Kwimba kimondo kilishuka mnamo mwaka 1930 waliokishuhudia kikishuka lazima walishangaa wakidhani ni moto unaoshuka kutoka mbinguni.

Baadhi ya mataifa yaliyoendelea yana programu maalum za Utafiti wa anga.

Na wanatumia tafiti hizo kujijenga kiulinzi, dhidi ya uwezekano wa tishio la shambulio kutoka anga za mbali.

Hii ni kwa sababu mwanadamu hawezi kujidanganya kuwa dunia hii anayoishi ndio pekee yenye viumbe hai.

Kwa hiyo wanapanua pia uwezo wao wakutengeneza silaha, hasa zile za teknolojia ya juu.

Na pia wanatengeneza mashine zinazojiendesha zenyewe au kuendeshwa na watu bandia, Robots, kwa ajili ya kushughulika na silaha ambazo pengine watu wa kawaida wasiweze kuziendesha kwa ufanisi.

Tanzania ilikwisha wahi kuwa eneo zuri la jukwaa kwa ajili ya kuangalizia matukio ya anga za nje au “Unajimu.” (Astronomia).

Kwa mfano Kule rujewa mwaka 2016 ilikua ni fursa adimu kwa Dunia kushuhudia tukio adhimu la kupatwa kwa jua.

Katika  matukio haya ya astronomia kwa mfano kupatwa kwa jua au mwezi mara nyingi watu wengi hupenda kufahamu kile kinachojiri kwa maelezo rahisi ya sayansi.

Lakini huwa mambo hayo hayafafanuliwi kabisa na wanazuoni au wasomi na watafiti waliomo nchini.

Hii ni pamoja na kwamba wataalamu wa mambo hayo duniani wamebainisha wazi kuwa Tanzania ni nchi iliyokaa katika eneo zuri na muafaka Ki-Jiografia kwa Utafiti wa Mambo ya Anga na Unajimu.

Kuna mengi yanayoshawishi nchi ya Tanzania kujiunga kikamilifu katika harakati za unchunguzi wa Mambo ya anga japo bado hakuna taasisi au shirika rasmi la kufuatilia mambo hayo eneo hili.

Kwa sasa ni nchi za Kenya na Rwanda pekee Afrika Mashariki zenye satelite katika anga za mbali, huku Uganda nayo ikijiandaa kurusha yake mawinguni hivi karibuni.

Habari Zingine

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari